iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) –Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina (Hamas) amependekeza mfumo mpya wa uongozi wenye kujumuisha wote ili kupatikane umoja wa kitaifa Palestina.
Habari ID: 3472914    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/30

TEHRAN (IQNA)- Israel inashinikizwa na jamii ya kimataifa isitishe mpango wake wa kupora maeneo zaidi ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472895    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/24

TEHRAN (IQNA)- Nchi mbali mbali duniani zinaendelea kupinga utekelezaji wa mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupora eneo kubwa la Ukingo wa Magharibi.
Habari ID: 3472878    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/19

TEHRAN (IQNA) –Mamia ya watu wameshiriki katika maandamano mjini Amsterdam Uholanzi Jumapili na kutangaza kuunga mkono Wapalestina huku wakipinga mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel kupora ardhi zaidi za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472865    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/15

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) amewatumia barua tofauti wakuu na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu zaidi ya 40 akiwataka kuchukua hatua za harakati kusitisha mpango wa Israel wa kutaka kuyaunganisha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3472852    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/10

TEHRAN (IQNA) – Maafisa wa kijasusi wa utawala haramu wa Israel Ijumaa walimkamata Imamu wa Msikiti wa Al Aqsa Sheikh Ekrima Sabri akiwa nyumbani kwake Quds (Jerusalem) Mashariki.
Habari ID: 3472814    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/29

Sayyed Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Kaitbu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon uwepo wa majeshi ya Marekani katika eneo umetokana na kuimarika nguvu za harakati za mapambano ya Kiislamu au muqawama.
Habari ID: 3472806    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/27

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema hakuna shaka kuwa utawala wa Israel utasambaratika na amesisitiza kuwa, vita asili vitakuwa na Marekani.
Habari ID: 3472793    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/23

TEHRAN (IQNA) - Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amefuta makubaliano yote yaliyofikiwa kati ya mamlaka hiyo na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472786    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20

Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Intifadha ya taifa la Palestina imeshavuka mipaka ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuingia kwenye awamu itakayoamua hatima yake na akasisitiza kwamba: Minong'ono ya kufikia tamati Israel ghasibu inasikika kwenye mitaa ya Tel Aviv.
Habari ID: 3472784    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20

TEHRAN (IQNA) - Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imepasisha kwa kauli moja muswada wa dharura wa kukabiliana na njama na uhasama za utawala wa Kizayuni wa Israel, dhidi ya amani na usalama wa kieneo na kimataifa.
Habari ID: 3472759    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/12

TEHRAN (IQNA) – Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu yanatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii nchini Afrika Kusini, kutokana na janga la corona.
Habari ID: 3472758    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/12

TEHRAN (IQNA) - Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema Baraza la Usalama la umoja huo limefeli kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel utekeleza maazimio ya baraza hilo kuhusu Palestina na Syria.
Habari ID: 3472699    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/24

Kufuatia janga la corona
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa taasisi za za kisheria Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kuchukua hatua za dharura za kuwaokoa mateka Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472675    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/17

TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ichukue hatua za dharura za kuzuia hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel za kunyakua ardhi zaidi Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3472661    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/13

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema harakati hiyo imeazimia kuhakikisha kuwa mateka wa Kipalestina walioko katika vizuizi vya utawala wa Kizayuni wa Israel wanaachiwa huru katika mpango wa kubadilishana wafungwa na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3472652    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/10

TEHRAN (IQNA) - Kuna uwezekano Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameambukizwa ugonjwa hatari wa COVID-19 au corona baada ya vipimo vya mshauri wake wa karibu kuonesha amekumbwa na maradhi hayo yanayoenenea kwa kasi duniani
Habari ID: 3472617    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/30

TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na asasi zingine za dunia kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel uwaachilie huru Wapalestina inaowashikilia katika magereza yake ili wasiambukizwe ugonjwa wa COVID-19 au corona ambao umeenea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).
Habari ID: 3472601    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/25

TEHRAN (IQNA) - Utawala wa Kizayuni wa Israel umemkamata Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Wakfu wa Kiislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) huku kukiwa na tetesi kuwa Wazayuni wanalenga kumuambukjiza kirusi cha corona.
Habari ID: 3472571    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/16

Makundi ya Palestina
TEHRAN (IQNA) –Makundi ya muqawama au kupigania ukombozi wa Palestina yamesisitiza kuwa, matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge katika utawala wa Kizayuni wa Israel yanayoneysha kuwa hakuna mabadiliko yoyote katika sera za utawala huo.
Habari ID: 3472526    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/03