iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Jumamosi ya jana ilishuhudia siku ya sita tokea utawala wa Kizayuni wa Israel unazishe hujuma ya kinyama dhidi ya Wapalestina katika eneo la Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3473914    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/16

TEHRAN (IQNA)-Raia Wapalestina 133, wakiwemo sita wa familia moja, wameuawa katika mashambulio ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza.
Habari ID: 3473913    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/15

TEHRAN (IQNA)- Miaka 73 iliyopita, utawala bandia wa Israel ulitangaza uwepo wake baada ya kufanya mauaji makubwa ya umati dhidi ya Wapalestina. Siku hii inajulikana kama Siku ya Nakba.
Habari ID: 3473912    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/15

TEHRAN (IQNA)- Tawi la kijeshi la Harakati ya Mapamabno ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) limevurumisha mamia ya makombora katika miji ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kusababisha hasara kubwa.
Habari ID: 3473909    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/14

TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Kenya jana waliandamana katika mji mkuu, Nairobi na kubainisha uungaji mkono wao kwa Wapalestina ambao wanakabiliwa na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Habari ID: 3473907    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/14

TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Afya ya Ukanda wa Ghaza ilikuwa imetangaza kuwa, wananchi 87 wa Palestina wameshauawa shahidi kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni.
Habari ID: 3473905    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/13

TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Wazayuni makatili na wauaji hawana uhusiano na dini yoyote ile.
Habari ID: 3473903    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/12

TEHRAN (IQNA)- Mabalozi wa kudumu wa nchini wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika Umoja wa Mataifa wametangaza azma yao ya kuhamisisha jamii ya kimataifa iunge mkono taifa la Palestina ambalo linakabiliwa na hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473899    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/11

TEHRAN (IQNA)- Sheikh mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri ametoa taarifa na kulaani ‘ugaidi wa Kizayuni’ baada ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel kuwahujumu Wapalestina katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds.
Habari ID: 3473892    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/09

TEHRAN (IQNA)- Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo pia ilikuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ilishuhudia hujuma mpya askari wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3473891    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/09

TEHRAN (IQNA)- Ijumaa iliyopita tarehe 7 Mei askari wa utawala haramu wa Israel walivamia msikiti mtakatifu wa al-Asqa katika mji wa Quds (Jerusalem). na kuwapiga kikatili Wapalestina waliokuwa wanatekeleza ibada zao katika msikiti huo. Shirika la Hilali Nyekundu ya Palestina limesema Wapalestina wasiopungua 205 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.
Habari ID: 3473890    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/09

TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali hujuma ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa wakati Wapalestina walipokuwa katika eneo hilo takatifu.
Habari ID: 3473887    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/08

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, harakati ya kuporomoka na kutoweka utawala wa Kizayuni imeanza na haitasimama; na akawahutubu Mujahidina wa Palestina kwa kuwaambia: "Endelezeni mapambano halali dhidi ya utawala ghasibu ili ulazimike kukubali kura ya maoni."
Habari ID: 3473886    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/07

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unakaribia mwisho wa uhai wake.
Habari ID: 3473885    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/07

TEHRAN (IQNA)- Siku ya Kimataifa ya Quds katika mwaka huu wa 2021 inaadhimishwa huku kukiwa kunashuhudiwa matukio muhimu katika medani za kisiasa za hararkati za muqawama au mapambano ya Kiislamu kwa upande mmoja na mikakati ya kuanzishwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel katika upande wa pili.
Habari ID: 3473882    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/06

TEHRAN (IQNA)- , Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria siku ya Kimataifa ya Quds inayoadhimishwa Ijumaa na kusema: "Wiki hii tuna Siku ya Quds. Hii ni siku ambayo ni fakhari kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni kati ya wosia wa Imam Khomeini (MA).
Habari ID: 3473880    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/05

TEHRAN (IQNA) -Makundi ya muqawama na kupigania ukombozi wa Palestina yametoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuchukua hatua zozote za kuwakandamiza vijana Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473877    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/04

TEHRAN (IQNA) - Utawala wa Kizayuni wa Israel unajaribu kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa Bunge la Palestina katika mji wa Quds (Jerusalem) hatua ambayo imekabiliwa na tahadhari kutoka kwa makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3473853    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/27

TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa kulaani hatua za kijinai walizofanyiwa hivi karibuni wananchi wa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na kusisitiza mshikamano wake na taifa tukufu la Palestina.
Habari ID: 3473844    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/24

TEHRAN (IQNA)- Mlipuko mkubwa umejiri katika kiwanda nyeti cha utawala wa Kizayuni wa Israel ambacho hutumika kutengeneza makombora.
Habari ID: 3473840    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/22