IQNA – Idhaa ya Qur’ani Tukufu ya Misri, yenye makao yake Cairo, imeanza kurusha hewani usomaji wa Qur’ani kwa mtindo wa tarteel wa miaka ya 1960 wa qari mashuhuri Sheikh Mohamed Siddiq El‑Minshawi.
IQNA – Nchi kadhaa za Kiislamu zimelaani vikali kuvamiwa kwa viwanja vya Msikiti wa Al‑Aqsa na walowezi wa Kizayuni wa Israel katika Al‑Quds (Jerusalem) ya Mashariki iliyo chini ya ukaliaji mwishoni mwa wiki hii.
IQNA – Chuo cha Kimataifa cha Al-Azhar nchini Misri kiliandaa programu ya ziara ya maimamu, wahubiri na walinganiaji wageni kutembelea vivutio vya kihistoria vya Kiislamu na Kikristo katika eneo la Fustat.
IQNA – Wakiwa na mizigo mikononi mwao lakini nyoyo zao zikiwa bado zimejaa athari za ibada za Hija, mahujaji waliokuwa wakiondoka walikabidhiwa kila mmoja zawadi yanakala ya Qur’ani Tukufu.
IQNA – Raundi ya fainali ya Mashindano ya Qur’ani yanayorushwa mubashara kupitia televisheni, “Inna lil-Muttaqina Mafaza” (Hakika kwa wachamungu ipo mafanikio/maokoleo), inatarajiwa kufanyika baadaye wiki hii.
IQNA – Kwa kuanzisha akademia ya Qur’ani, madada wawili mjini Pristina, mji mkuu wa Kosovo, wameweza kuwafundisha mamia ya watoto namna ya kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu kupitia miaka yao ya juhudi na bidii.
IQNA – Kwa lengo la kuizidisha safari ya kiroho ya mamilioni ya wanaouzuru Msikiti wa Mtume au Al Masjid An Nabawi huko Madina Al-Munawwara, umeanzishwa mpango wa mwongozo kwa wageni unaounganisha ukunjufu wa mapokezi na mafundisho ya dini.
IQNA – Idara ya Mfawidhi au Msimamizi wa wa Haram Tukufu ya Imam Ali (AS) mjini Najaf, Iraq, Jumapili imetangaza kuanza kwa shughuli za Wiki ya 15 ya Kimataifa ya Ghadir.
IQNA – Wengi wanaamini kuwa kurekodiwa kwa Surat Yusuf kulikuwa mgeuko wa kweli katika maisha ya Sheikh al-Sayyid Saeed, na mafanikio hayo makubwa yakamfanya ajipatie umaarufu na hatimaye kunyakua lakabu inayostahiki ya “Sultan al-Qurra” (Mfalme wa Wasomaji Qur’ani).
IQNA – Video iliyosambazwa mtandaoni ikimuonesha Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, akisoma aya za Qur’ani Tukufu ndani ya Msikiti wa Aya Sofya mjini Istanbul, imepokelewa vyema na watumiaji wa mitandao ya kijamii.
IQNA – Katika vituo vya kuondokea abiria vya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Abdulaziz uliopo Jeddah, kuna jitihada tulivu na yenye baraka zinazoendelea.
IQNA – Wizara ya Awqaf (Wakfu) ya Misri imeuhuisha na kuuenzi ukumbusho wa qari marehemu wa Qur’ani Tukufu, Sheikh Sayyid Abdul Shafi Hilal, katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.