IQNA – Vijana wa Iran, wakiinua bendera ya nchi yao kwa fahari, wanajifunza na kutekeleza kwa vitendo jukumu la kulinda Mapinduzi ya Kiislamu wakiwa uwanjani na katika medani ya utumishi wa taifa.
IQNA – Wakati watu madhlumu wa Palestina na mataifa mengi ya Kiislamu wakiwa chini ya dhuluma na uvamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel, baadhi ya nchi za Kiarabu zimeimarisha uhusiano wao wa siri na utawala huo wenye laana na nuksi; tabia ambayo Qur’ani Tukufu imeiashiria kwa onyo kali sana.
IQNA-Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) limelaani shambulio la Marekani na Israel dhidi ya Shule ya Shajareh Tayyebeh katika mji wa Minab, kusini mwa Iran, ambapo angalau wanafunzi na wafanyakazi wa shule 175 waliuawa katika mauaji ya kikatili tarehe 28 Februari.
IQNA-Jeshi la Yemen limetangaza kuwa liko tayari kuingilia moja kwa moja kijeshi iwapo pande nyingine zitaungana na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mhimili wa Muqawama.
IQNA-Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema mauaji ya wanafunzi katika Shule ya Minab yaliyotekelezwa na Marekani na Israel ni “sehemu ndogo tu ,” ya jinai ya kivita unaofanywa na muungano huo wa kijeshi wa tawala hizo mbili.
IQNA-Rais wa Iran amesema katika mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Malaysia kwamba nchi za Kiislamu hazipaswi kuwaruhusu maadui kupanda mbegu za mifarakano na kuwasha moto wa vita.
IQNA – Aya ya 39 ya Surah Al‑Hajj katika Qur’ani Tukufu inaeleza kwamba Waislamu wanapaswa kufanya yale yaliyo ndani ya uwezo wao, kisha wasubiri nusura ya Mwenyezi Mungu.
IQNA – Wananchi wa Iran, wakionyesha uungaji mkono wao kwa Mapinduzi ya Kiislamu, wameshiriki katika mijumuiko mbali mbali ya kuomba dua kwa ajili ya ushindi na kufanikiwa kwa wapiganaji wa Kiislamu.
IQNA – Wakati Salwan Momika, anayejulikana kwa vitendo vya kuchoma na kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu hadharani nchini Uswidi, alipoingia katika duka la mfanyabiashara Mkristo, hakupokelewa kwa huduma bali kwa kukataliwa ambapo mmiliki wa duka alikataa kumuuzia bidhaa na mara moja akamuamuru atoke nje.
IQNA – Kituo cha Kiislamu cha AlAzhar nchini Misri kimehimizwa kufikiria upya msimamo wake kuhusu mashambulizi yanayoendelea ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, na pia kutafakari kwa makini kuhusu mustakabali wa ulimwengu wa Kiislamu na Umma wa Waislamu.
IQNA – Serikali ya Kiislamu haianzi vita dhidi ya yeyote, lakini ina wajibu wa kujibu uchokozi, fitina na vitendo vya kueneza hofu ili msaada wa Mwenyezi Mungu uweze kuifikia.
IQNA – Sayyid Ammar al‑Hakim, kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Kitaifa ya Iraq, amelaani vikali shambulio la Marekani dhidi ya makao makuu ya Vikosi vya Kujitolea vya Umma (PMU) katika jimbo la Anbar.
IQNA – Iran ni nchi ambayo viongozi, maafisa wa serikali na makamanda wa kijeshi hawasimami kutoa heshima kwa majeneza ya wanajeshi wao; badala yake mara nyingi wao hutangulia kuuawa shahidi, kisha wananchi wa nchi yao ndio huwapa mazishi na kuwaaga kwa heshima.
IQNA-Kama ilivyokuwa kwa Nabii Ya‘qub (A.S.) alipoweka sharti la kuchukua ahadi thabiti mbele ya Mwenyezi Mungu kabla ya kumruhusu Benyamini aondoke, vivyo hivyo kuja kwa Mwokozi aliyeahidiwa kunahitaji ahadi nzito na ya kweli kutoka kwa Umma unaomsubiri.
IQNA-Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini Kenya, Shakira Wafula, ametangaza mshikamano wake na watu wa Iran na Palestina, akitoa ujumbe wa imani na matumaini.