IQNA

Siku ya Quds

Nasrallah: Harakati za Muqawama zitapata 'ushindi mkubwa' katika vita dhidi ya Israel

6:20 - April 06, 2024
Habari ID: 3478636
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema mhimili wa muqawama una uhakika wa kupata "ushindi mkubwa" katika vita vyake vinavyoendelea dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Sayyed Hassan Nasrallah aliyasema hayo katika hotuba yake ya televisheni iliyotangazwa jana Ijumaa katika mji mkuu Beirut kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds. Tukio hilo la kuunga mkono Palestina hufanyika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka kwa kuzingatia wito wa marehemu muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imam Khomeini.

Nasrallah alisema,  "Tutaendeleza vita hadi pale muqawama na Wapalestina wa Gaza watakaposhinda." Ameongeza kuwa:  "Tunakabiliwa na tukio ambalo limeweka maisha ya Israeli katika hatari na kufichua udhaifu wake."

Harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu katika eneo zima, zikiwemo Lebanon, Iraq na Yemen, zimekuwa zikifanya mashambulizi ya kijasiri dhidi ya maeneo ya utawala wa Israel na wafuasi wake tangu Oktoba 7, wakati utawala huo ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.

"Jambo muhimu ni kwamba tusimame kidete na kuwa imara huko Gaza, Ukingo wa Magharibi [unaokaliwa kwa mabavu], Lebanon, Yemen, na Iraq," amesema Kiongozi wa Hezbollah na kubaini kuwa: "Hivi ni vita ambavyo tunaelekea kupata ushindi.".

Kiongozi wa Hizbullah alipongeza Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa Storm, ya kulipiza kisasi ya harakati za muqawama huko Gaza ambaye ilipelekea utawala katili wa Israel uanzishe vita vya mauaji ya kimbari.

Sayyed Hassan Nasrallah amebainisha kuwa, licha ya vita vya miezi sita dhidi ya Gaza, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameacha kutambua malengo yote aliyokuwa akitaka kuyafikia kupitia kampeni hiyo ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kuyatokomeza makundi ya muqawama ya Gaza na kuwarejesha wale waliokuwa kuchukuliwa mateka na harakati za muqawama wakati wa Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa.

Wakati huo huo kiongozi huyo wa Hizbullah ameashiria shambulio la hivi karibuni la kigaidi la utawala wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria Damascus na kusababisha vifo vya maafisa saba wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Sayyed Hassan Nasrallah amesema: "Kuwa na uhakika kwamba majibu ya Iran kuhusu suala la ubalozi mdogo wa Iran yatakuja bila shaka."

3487817

 

captcha