Katika taarifa kufuatia kuharibiwa turathi za binadamu nchini Syria na hatari inayoukabili mji wa kihistoria wa Palmyra nchini humo, amesema kuharibu, kuiba na kuuza turathi za kali na za kihistoria ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
Sheikh Ahmad Tayyib amesisitiza kuhusu udharura wa kulinda athari za turathi ya historia ya mwanaadamu nchini Syria baada ya magaidi wa kundi la Kiwahabi na Kitakfiri la Daes au ISIS kutekeleza uharibifu dhidi ya turathi hizo za kale. Mkuu wa Al Azhar ameitaka jamii ya kimataifa ichukue hatua kulinda athari za kale Syria ili zisikumbwa na hatima ya athari za kale Libya na Iraq ambazo ziliharibiwa na magaidi.
Kwingineko Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limewaua kwa halaiki raia 400 wa Syria, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto katika shambulio dhidi ya mji wa kale na wa kihistoria wa nchi hiyo wa Palmyra. Televisheni ya Syria imeripoti jinai hiyo iliyofanywa na magaidi hao wanaoungwa mkono na madola ya kigeni ikiwanukuu wakaazi wa mji huo wa kihistoria wenye magofu ya kale yaliyohifadhiwa vizuri ya tokea enzi za utawala wa Rumi yakiwemo mahekalu.../mh