IQNA

19:09 - March 31, 2020
News ID: 3472619
TEHRAN (IQNA) -Rais Joko Widodo wa Indonesia ametangaza hali ya hatari kitaifa nchini humo kufuatia kuenea ugojwa wa COVID-19 au corona huku akitangaza hatua za kuwasiadia watu wenye kipato cha chini.

Hatua ambazo zimechukuliwa zinajumuisha kuwapa misaada ya chakula wale ambao watapoteza pato kutokana na sharia ya kuwataka watu kukaa majumbani. Aidha serikali ya Indonesia imesema itawapunguzia wananchi malipo ya umeme katika kipindi cha hali ya hatari. Halikadhalika katika hatua nyingine ya kukabiliana na kuenea ugonjwa wa corona, serikali ya Indonesia imesema itawaachilia huru wafungwa 30,000 ili kupungumza msongamano katika magereza ya nchi hiyo.

Hadi sasa watu 1,414 wameambukizwa corona nchini Indoneisa na miongoni mwao 122 wamefarikia dunia. Maafisa wa afya wanasema ukosefu wa vipimo ni jambo ambalo limefunika ukweli kuhusu walioambukizwa.

3471009

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: