Wayemen hufanya maandamano siku ya Ijumaa, wakiwa wamebeba bendera za Yemen, Palestina, na Lebanon na picha za wale waliouawa shahidi katika mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya nchi za kikanda.
Walisisitiza mshikamano wao na taifa la Syria katika kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Israel na kukalia kwa mabavu sehemu ya ardhi ya Syria baada ya kuanguka kwa serikali ya Bashar al-Assad.
Waandamanaji hao wa Yemen pia wamezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kusitisha jinai na mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
Walisisitiza msimamo usiobadilika wa Yemen katika kuliunga mkono taifa la Palestina na wapiganaji wa muqawama.
Wakati huo huo, Jeshi la Yemen limetangaza kutekeleza operesheni tatu za ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel kwa ajili ya kuiunga mkono Palestina.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, operesheni za Yemen dhidi ya adui Mzayuni zitaendelea hadi pale vita dhidi ya Ghaza na mzingiro wa eneo la Palestina utakapokoma.
3491040