IQNA

Kadhia ya Palestina

Chuo Kikuu Jordan chakosolewa kwa kuwakandamiza wanafunzi wanaounga mkono Palestina

21:30 - November 08, 2024
Habari ID: 3479720
IQNA - Chuo Kikuu cha Hashemite cha Jordan kimeshutumiwa kwa kuwakandamiza wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina.

Chuo kikuu hivi karibuni kimetishia hatua za kinidhamu dhidi ya wanafunzi wanaohudhuria mikutano ya kuwaunga mkono Wapalestina wa Gaza wanaokabiliwa na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kituo cha haki za binadamu cha Ahrar kimeripoti kuwa wanafunzi wasiopungua 15 wamepokea onyo hilo.
Hatua hiyo imeibua wimbi la ukosoaji na hasira, huku wengi wakisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba majaribio ya kuwanyamazisha watu yakomeshwe.
Mohamed Ramzi Khatib, mwanafunzi wa Jordan, alisema vyama vya siasa vinakuja vyuo vikuu vinapohitaji wanafunzi kushiriki katika shughuli za kisiasa lakini hivi sasa viko kimya juu ya kukandamizwa kwa wanafunzi wanaotoa sauti ya mshikamano na Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Alisema katika chapisho kwenye X kwamba maonyo yaliyotolewa kwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Hashemite ni ya hivi punde tu katika safu ya hatua kama hizo katika vyuo vikuu vya kibinafsi na vya umma tangu Oktoba iliyopita.
Mwanafunzi mwingine aliandika kwenye X kwamba majaribio ya kuwanyamazisha waandamanaji na kukandamiza sauti ya ukweli yatashindwa.
Serikali ya Jordan, ambayo inalaumiwa kuwa kibaraka wa Marekani, imeweka vikwazo vingi kwa shughuli zinazoiunga mkono Palestina huku utawala wa Israel ukiendeleza ukatili wake huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

3490599

Habari zinazohusiana
captcha