IQNA

Watetezi wa Palestina

Wananchi wa Magharibi wasema hakuna Krismasi kwa sababu ya mauaji ya kimbari Gaza

18:25 - December 24, 2023
Habari ID: 3478086
IQNA - Mikutano ya hadhara imefanyika katika miji katika nchi mbalimbali za Magharibi mwishoni mwa juma kupinga mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza na kutaka kuwasilishwa kwa misaada ya kibinadamu katika eneo lililozingirwa.

Miji ya Paris, Berlin, London, New York, Sydney, na Melbourne ilishuhudia maandamano yenye shauku ya kuhimiza mshikamano na Wapalestina wanaodhulumiwa.

Mamia walikusanyika mjini Paris chini ya kauli mbiu: "Hakuna Krismasi huko Gaza" kulaani vita vinavyoendelea katika eneo lililozingirwa.

Olivia Zemor, mwanaharakati wa kisiasa wa Ufaransa na rais wa Jumuiya ya Euro-Palestina iliyoandaa maanamano ya Parist alisisitiza juu ya ulazima wa kuandaa maandamano zaidi ya Wapalestina mwanzoni mwa mwaka mpya .

"Kwa upande wetu, tuna jukumu la kuwafahamisha watu hawa kwamba hawako peke yao na kwamba wanaungwa mkono na mamilioni ya raia katika nchi zote," alisema.

"Tunarudia, watu wa Palestina wanapitia wakati mgumu zaidi za historia yao ndefu, na madola makubywa dunaini yakiongozwa na Biden na Macron yamewapuuza," Zemor aliongeza.

Waandamanaji wamelaani mauaji ya waandishi wa habari, madaktari na wanasheria yaliyofanywa na jeshi la Israel na kimya cha ulimwengu kuhusu mauaji hayo ya kimbari.

Pia walirudia kusema: "Israel muuaji, Macron ni mshirika wa mauaji" na "Palestine Huru," huku wakihimiza kususia Israeli na wale wanaoisaidia dhidi ya raia wa Palestina.

Mjini Berlin, maandamano yenye nguvu ya Wapalestina yaliwaleta pamoja mamia, wakikusanyika kutoka Kreuzberg hadi kwenye lango mashuhuri la Brandenburg, yakiunga mkono wito wa "Mshikamano na Palestina."

Huko London, wanaharakati waliandaa maandamano kwenye Mtaa wa Oxford wakati wa shamrashamra za ununuzi wa Krismasi, wakihimiza kususiwa kwa bidhaa "zinazohusishwa na Israeli". Nyimbo za "Palestina huru" zilisikika huku wanaharakati wakitoa wito wa kuwepo ufahamu wa wateja ili wasusie bidhaa zinazohusishwa na Israel.

Wakati huo huo, kote Australia, kutoka kwa msafara wa Melbourne unaodai usitishaji wa kudumu wa Gaza hadi maandamano makubwa ya Sydney kupita Kanisa kuu la St Mary's, mwito wa kukomesha uvamizi wa kijeshi wa Israeli uliongezeka.

Maandamano ya hadhara pia yaliandaliwa kote Marekani huku kukiwa na msukosuko wa ununuzi wa siku za mwisho wa sikukuu. Waandamanaji walisema kuna udharura la kusitishwa kwa mapigano na misaada zaidi ipelekwe Gaza ili kupunguza mateso yaliyosababishwa na vita vya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina.

Waandamanaji wanaounga mkono Palestina pia waliingia katika mitaa ya Ottawa, mji mkuu wa Kanada kulaani vita vinavyoendelea Israel katika Ukanda wa Gaza.

No Xmas as Usual during Genocide: Pro-Palestine Rallies Held in Western Countries

No Xmas as Usual during Genocide: Pro-Palestine Rallies Held in Western Countries

No Xmas as Usual during Genocide: Pro-Palestine Rallies Held in Western Countries

Pro-Palestine rally in Paris calls for end to Gaza massacre

 

Habari zinazohusiana
captcha