IQNA

15:40 - October 27, 2020
News ID: 3473301
TEHRAN (IQNA)- Watu saba wameuawa wakiwa katika darsa ya Qur’ani Tukufu katika hujuma iliyotekelezwa mjini Peshawar, kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Kwa mujibu wa taarifa mbali na watu saba kuuawa wengine 72, wakiwemo watoto kadhaa walijeruhiwa katika hujuma hiyo.

Taarifa imesema mlipuko umejiri mapema Jumanne asubuhi katika Msikiti wa Jamia wa Speen, ambao pia hutumika kama chuo cha kidini kwa ajili ya wakaazi wa mtaa wa Dir Colony.

Mkuu wa polisi mjini Peshawar Mohammad Ali Khan amesema wanafunzi walikuwa wanasoma Qur’ani wakati wa kujiri mlipuko. Amesema ataarifa za awali zinaonyesha bomu lenye uzito wa kilo tano lilitumika katika hujuma hiyo ya kigaidi.

Hakuna kundi lololote ambalo limedai kuhusika na hujuma hiyo. Magaidi wa kufurishaji wa Tehreek-e-Taliban wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya kigaidi amra kwa mara Pakistan dhidi ya raia na maafisa wa usalama.

3472946

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: