IQNA

Msikiti wa Al Aqsa

Utawala wa Israel kufadhili uvamizi wa walowezi wa Msikiti wa al-Aqsa

17:18 - August 27, 2024
Habari ID: 3479334
IQNA - Utawala wa Israel umetangaza mpango wa kufadhili walowezi haramu wa Israel kuvamia Msikiti wa al-Aqsa katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la al-Quds (Jerusalem) katika hatua nyingine ya uchochezi inayolenga eneo hilo la tatu kwa utakatifu katika Uislamu.

Kwa mujibu wa taarifa, ofisi ya waziri wa turathi mwenye msimamo mkali Amichai Eliyahu itatenga nusu milioni dola  kwa mradi huo, unaotarajiwa kutekelezwa katika wiki zijazo.

Wizara hiyo inafanya uratibu na ile inayoitwa wizara ya usalama, inayoongozwa na Waziri mwenye misimamo mikali sana Itamar Ben-Gvir, kupata kibali cha polisi kwa ziara hizo zinazofadhiliwa.

Mapema Jumatatu, Ben-Gvir aliiambia Redio ya Jeshi la utawala wa Israel kwamba Wayahudi wana haki ya kutekeleza ibada za Kiyahudi katika Msikiti wa Al-Aqsa na alionyesha nia ya kujenga sinagogi katika eneo hilo.

Hii ni mara yake ya kwanza kujadili kwa uwazi kujenga sinagogi huko, ingawa mara kwa mara ametoa wito wa kuruhusu maombi ya Kiyahudi kwenye tovuti hiyo.

Msikiti wa Al-Aqsa unachukuliwa kuwa eneo la tatu takatifu katika Uislamu.

Chini ya hali ya miongo kadhaa ya zamani inayodumishwa na mamlaka ya Israel, Wayahudi na watu wengine wasio Waislamu wanaruhusiwa kuzuru eneo la Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu wakati wa saa maalum, lakini hawaruhusiwi kusali hapo au kuonyesha alama za kidini.

Ben-Gvir pia amekosolewa na baadhi ya Wayahudi wa Orthodox, ambao wanaona msikiti huo kuwa eneo takatifu la Waislamu na Wayahudi hawapaswi kuingia. Kwa mujibu wa ma-Rabi wakuu, ni haramu kwa Myahudi yeyote kuingia sehemu yoyote ya Al-Aqsa kutokana na utakatifu wake.

Katika miaka ya hivi karibuni, vizuizi katika jumba hilo vimezidi kupuuzwa na watu wenye msimamo mkali wa kidini kama Ben-Gvir, wakati mwingine na kusababisha makabiliano na Wapalestina.

Msikiti wa Al-Aqsa unasimamiwa na Jordan, lakini usimamizi wa wanaoingia eneo hilo uko mikononi mwa vikosi vya utawala ghasibu wa Israel

3489669

Habari zinazohusiana
captcha