TEHRAN (IQNA)- Mitandao ya Iraq imesembaza klipu ya marhum Ayatullahil Udhma Sayyid Mohammad Saeed Tabatabai Hakim akiwa katika matembezi ya Arobaini ya Imam Hussein AS katika miaka ya nyuma.

Ayatullah Sayyid Mohammad Saeed Tabatabai Hakim Marjaa Taqlid maarufu katika mji wa Najaf al Ashraf nchini Iraq aliaga dunia Ijumaa kutokana na mshtuko wa moyo.
Kwa mujibu wa taarifa alikuwa amefanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali moja mjini Najaf kabla ya kuaga dunia Ijumaa.
Ayatullah Saeed Hakim alikuwa mmoja kati ya Marjaa Taqlid wanne wa Kishia mjini Najaf. Ameandika vitabu zaidi ya 40 kuhusu Fiqhi ya Kiislamu na amewafunza wanazuoni wengi katika fani mbali mbali za Kiislamu.
Mwendazake alizaliwa katika familia ya maualmaa wa Kiislamu mjini Najaf mwaka 1354 Hijria Qamari (1936) na alikuwa mjukuu wa marhum Ayatullahil Udhma Muhsin al Hakim.