IQNA

Msikiti wahujumiwa Calgary, waumini waingiwa na hofu

22:14 - September 13, 2021
Habari ID: 3474290
TEHRAN (IQNA)- Wizi katika msikiti huko Calgary nchini Canada umepelekea waumini waingiwe na hofu na wasiwasi mkubwa.

Kati ya saa  moja unusu na saa mbili usiku Jumamosi, mwanamume aliyekuwa akiendesha lori aliwasili katika Kituo cha Kiislamu cha  Hussaini huko Kalgary, na kuharibu lango na kuvunja kufuli kabla ya kuingia eneo la ndani ambalo pia linajumuisha msikiti.

Alipokuwa ndani, aliiba Televisheni, mfumo wa vipaza sausi, projekta,  mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo vinaweza kufikia  thamani ya dola  5,000, alisema Riyaz Khawaja, mdhamini wa jumuiya hiyo..

Mwizi huyo pia aliharibu milango kadhaa wakati wizi huo katika uhalifu ambao sasa unachunguzwa sasa na polisi wa jiji, alisema.

Khawaja alisema hakuna dalili kwamba uhalifu huo unahusiana na chuki, ingawa alibaini ulitokea kwenye kumbukumbu ya miaka 20 ya shambulio la kigaidi la 9/11 huko Marekani.

Alisema wizi huo umetikisa Waislamu wa eneo hilo, akibainisha kuwa tukio hilo lilijiri dakika chache kabla ya kikundi cha wanawake kuwasili kwa ajili ya shughuli ya kidini.

Mashambulio mengi dhidi ya Waislamu nchini Canada yameripotiwa katika miezi ya hivi karibuni huku viongozi wa Kiislamu wakitaka usalama uimarishwe misikitini.

3475699

Kishikizo: msikiti canada waislamu
captcha