IQNA

Waisilamu Canada washtuka baada ya kupokea vitisho, barua ya ubaguzi

22:26 - September 03, 2021
Habari ID: 3474254
TEHRAN (IQNA)-Wanachama wa Kituo cha Kiislamu cha Langley huko Langley, British Columbia nchini Canada, "wameshtuka" na "wamekata tamaa" baada ya kupokea barua ya vitisho na ya kibaguzi.

Barua hiyo ilitumwa na mtu asiyejulikana mnamo Agosti 26 na inatoa madai ya kutishia ya kutaka kituo hicho kufungwa katika kipindi cha miezi miwili. Barua hiyo inataja Inarejelea shambulio la msikiti wa mjini Christchurch, ambapo mtu mwenye itikadi kuwa wazungu ndio wanaadamu bora aliua waumini 51 katika misikiti miwili wakati wa Sala ya Ijumaa huko New Zealand, mnamo Machi 15, 2019.

"Hisia ambayo tulipata mwanzoni ilikuwa ya karaha na mshtuko. Sidhani kama watu wanaamini tunaishi katika ulimwengu ambao mambo kama haya bado yapo. Watu wamekasirika, watu wengine wana hasira," alisema Imam Fawad Kalsi wa Kituo cha Kiislamu cha Langley.

Polisi ya Canada imetangaza kuwa inachunguza tukio hilo.

Fatema Abdalla wa Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Canada anasema Canada iko katikati ya mgogoro wa chuki, ubaguzi wa kimfumo na Islamophobia au chuki dhidi ya Uislamu..

"Inatosha, jamii zetu hazipaswi kuwa na hofu hii ya kuwa mlengwa, haswa katika maeneo yetu ya ibada," alisema.

"Tumeona uharibifu wa mara kwa mara kwenye sehemu za ibada ... tumeona mashambulio kwa familia yetu ya London ... tumeona mashambulio kwa wanawake wa Kiislamu wenye asili ya Afrika huko Calgary na Edmonton .. na sasa tunaona vitisho hatari vinatolewa. "

Barua hiyo, ambayo iliandikwa kwa kutumia herufi zilizokatwa kutoka kwa jarida, inasema imetoka kwa "KKK."

Bi. Abdallah anasema, "hii inaonyesha hitajio la dharura la kufanya zaidi kote Canada, haswa linapokuja suala la kuongezeka kwa vikundi vya wazungu wenye misimamo kali wanao amini wao ni bora kuliko wanaadamu wote."

Ameongeza kuwa, Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Canada linataka hatua zaidi dhidi ya makundi ya wazungu wanaoamini wao ni bora. Anasema kuna zaidi ya makundi 250 ya wazungu wenye msimamo mkali nchini Canada na hivyo mpango wa kitaifa wa kukabiliana na tatizo hilo unahitajika.

Imam Fawad Kalsi  amesema hatua za usalama katika Kituo cha Kiislamu cha Langley, ambacho kina wanachama wapatao 500, zimeimarishwa ili kuhakikisha usalama na kila mtu, alisema.

"Dini yetu inatufundisha kuwa sisi sote ni ndugu, hata watu hawa watu walioandika barua hii ... ikiwa kuna maoni potofu juu ya imani yetu, kuna haja ya kuwaelimisha," ameongeza.

Bi. Abdalla anakubali elimu ni muhimu katika kupambana na shida hii inayoongezeka.

"Inatia wasiwasi sana kutembea mitaani na kutazama huku na kule kwa uangalifu kila wakati, kuhakikisha uko salama, lakini hii inaonyesha haja ya hatua zaidi za wanajamii, na serikali yetu."

Mkuu wa Polisi Langley ameomba msaada Kitengo cha Uhalifu wa Chuki na Timu Jumuishi ya Utekelezaji wa Usalama wa Kitaifa ili kuchunguza tukio hilo. Polisi pia inafanya kazi na uongozi wa kituo hicho Kiislamu kushughulikia wasiwasi wa usalama na kuandaa mikakati kuhusu mustakabali.

3475609

captcha