IQNA

Kanisa lililojengwa miaka 178 iliyopita Canada labadilishwa kuwa Msikiti

21:26 - September 26, 2021
Habari ID: 3474344
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa jamii ya Wauyghur Waturuki wanaoishi katika mji wa Toronto, Canada wamenunua jengo la kale ambalo lilikuwa Kanisa na kuligeuza kuwa Msikiti.

Kanisa la Mount Carmel ambalo lilijengwa mwaka 1873 na sasa bada ya kubadilishwa na kuwa Msikiti litajulikana kama Kituo cha Kiislamu na Kiutamaduni cha Jamii ya Wauyghur Waturuki Canada.

Katibu Mkuu wa Jamii ya Wauyghur Waturuki Canada, Itibar Artysh amesema  kanisa hilo sit u kuwa litakuwa msikiti bali pia litakuwa ni kituo cha kijamii.

Amesema Waislamu wa eneo hilo hasa Jamii ya Wauyghur Waturuki Canada wamekuwa wakihitajia Msikiti na eneo la shughuli zao za kijamii.

Amesema katika kituo hicho watoto watapata mafunzo ya Kiislamu na hasa darsa za Qur’ani Tukufu ili kuwazuia kuiga utamaduni wa Kimagharibi.

Kasisi wa mwisho wa Kanisa la Mount Carmel, Robin Wilkie, alihudhuria sherehe za kufunguliwa msikiti huo ambapo amebainisha furaha yake kuwa, baada ya miaka mingi bila kutumiwa, eneo hilo la ibada sasa litajaa waumini, hata kama ni wa dini nyingine.

Aghalabu ya Wauyghur Waturuki ni wahamiaji kutoka China ambapo wanasema wamekuwa wakikandamizwa katika nchi hiyo.

تبدیل کلیسای تاریخی به مسجد از سوی مسلمانان کانادا

تبدیل کلیسای تاریخی به مسجد از سوی مسلمانان کانادا

 

4000527/

Kishikizo: canada ، msikiti ، kanisa ، waislamu ، Wauyghur ، china
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha