IQNA

Kiongozi wa Ansarullah

Marekani, Uingereza na Israel ndio wahandisi wa vita dhidi ya Yemen

21:41 - March 26, 2022
Habari ID: 3475076
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani, utawala haramu wa Israel na Uingereza ndio wahandisi wa kushambuliwa na kukaliwa kwa mabavu taifa la Yemen tokea mwaka 2015 hadi sasa.

Sayyid Abdul Malik Badruddin Al-Houthi alisema hayo katika hotuba yake kupitia televisheni usiku wa kuamkia leo na kueleza kuwa: Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ndizo zinazotekeleza uvamizi huo wa Marekani, Israel na Uingereza.

Amesema misingi ya vita dhidi ya Yemen ni hulka na mienendo ya jinai, na uvamizi huo umelenga sekta zote za taifa hilo maskini la Kiarabu, mbali na kumwaga damu za Wayemen.

Sayyid Abdul Malik Badruddin Al-Houthi ameongeza kuwa, Yemen inakabiliwa na vita shadidi vya kiuchumi vinavyolenga kuharibu na kusambaratisha rasilimali zote za nchi hiyo, na kuitaabisha kila familia ya Yemen.

Moto wa vita uliowashwa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen kuanzia mwezi Machi 2015 na kuendelea hadi sasa umeshapelekea mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia kupoteza maisha, mbali na kuwaacha wengine zaidi milioni nne wakiwa hawana pa kuishi. 

Uchokozi na uvamzi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen umebomoa na kuharibu zaidi ya asilimia 85 ya miundombinu ya nchi hiyo masikini zaidi katika Bara Arabu na kuisababishia pia uhaba mkubwa wa chakula na dawa nchi hiyo ya Waislamu.

3478271

captcha