IQNA

Yemen yashambulia kituo cha mafuta Riyadh katika ulipizaji kisasi jinai za Saudia

14:17 - March 12, 2022
Habari ID: 3475031
TEHRAN(IQNA)-Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen ametoa ufafanuzi wa shambulio la ndege zisizo na rubani lililofanywa na jeshi la nchi hiyo ndani kabisa ya ardhi ya Saudi Arabia kujibu uchokozi na hujuma za kila leo wanazofanyiwa raia wa Yemen na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Riyadh.

Vita vya Yemen, sasa vimefikia kwenye hatua nyeti na hasasi mno, ambapo baada ya kupita zaidi ya miaka saba ya uvamizi wa muungano wa kijeshi wa Kiarabu na Kimarekani unaoongozwa na Saudi Arabia, jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi vimeshashika hatamu kwenye medani za vita za maeneo mbalimbali ikiwemo katikati na magharibi ya nchi hiyo, ambapo makombora na ndege zisizo na rubani za Yemen zimegeuka jinamizi kwa Wasaudi wavamizi.

Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen ameeleza katika taarifa kuwa, kikosi cha pamoja cha ndege zisizo na rubani cha jeshi na wapiganaji wa kujitolea kimefanya operesheni ya droni iitwayo "Uondoaji Mzingiro 1" hadi ndani kabisa ya ardhi ya Saudia, likiwa ni jibu kwa hujuma zinazozidi kuongezeka, mzingiro wa kidhalimu wa muungano wa Saudia dhidi ya wananchi wa Yemen na vilevile hatua ya muungano huo ya kuzuia meli zilizobeba bidhaa za mafuta zisiingie kwenye bandari za nchi hiyo.

4042024

Kishikizo: yemen saudia ansarullah
captcha