Abdulmalik Badruddin al-Houthi alisema Alhamisi katika hotuba yake kwamba: Kile ambacho adui wa Israeli anafanya Gaza, kwa ushahidi wa mashirika ya kimataifa, ni mauaji ya kimbari kwa maana halisi ya neno hilo; na kauli hiyo imetolewa namashirika ambayo hatujazoea kuyasikia yakizungumzia haki ipasavyo.
Kiongozi wa Ansarullah pia amesema kuwa, Marekani na 'Israel' zinafanya njama za kuudhibiti ulimwengu wa Kiislamu kwa njia ya mgawanyiko na ukandamizaji, akisisitiza umuhimu wa kuendelezwa muqawama na mapambano.
Abdul Malik al-Houthi amebainisha kuwa, utawala haramu wa Israel umefanya hujuma zaidi ya 180 nchini Lebanon, unaojumuisha mauaji, ubomoaji wa nyumba, na uharibifu wa mashamba, katika juhudi za kupata ushindi baada ya kufeli njama za kuisambaratisha Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.
Kiongozi huyo wa Harakati ya Wananchi ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, upanuzi unaoendelea wa uvamizi wa Israel nchini Syria,umedhibiti wa asilimia 95 ya mkoa wa Quneitra na kuelekea kusini mwa Damascus na Daraa.
Al-Houthi amesema kuwa, vikosi vya Wanajeshi wa Israel vimeweka vikwazo vikali kwa raia, kunyakua silaha, na kulenga rasilimali muhimu za maji ili kuendeleza malengo yao ya Israel ya kujitanua.
Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen aliendelea na hotuba yake akisema, "Kile ambacho adui wa Israel ameruhusu kuingia Gaza ni malori 12 pekee ndani ya siku 70." Vile vile ameashiria vita vya uadui wa Israel dhidi ya hospitali za kaskazini mwa Gaza na kusema, "Vita vya uadui wa Israel dhidi ya hospitali vimeshadidi."
4256365