IQNA

Yemen yasema itatoa jibu kali kwa ukiukaji mapatano ya usitishaji vita

11:47 - April 25, 2022
Habari ID: 3475165
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa, jeshi la Yemen na kamati za wananchi zitatoa jibu kali kwa ukiuka wa makubaliano ya kusitisha vita, akigusia vitendo viovu vya muungano wa vita unaoongozwa na Saudia huko Ma'rib.

Jumanne iliyopita, mamluki wa muungano vamizi wa Saudia walirusha makombora mawili ya Katyusha katika vituo vya jeshi na harakati ya Ansarullah huko Mashariki mwa Al-Balq katika mkoa wa Ma'rib na kukiuka makubaliano ya kusitisha vita mara sita kwa kushambulia nyumba za raia na ngome za jeshi katika mikoa ya Ma'rib na Lahj. 

Mohammed Abdul Salam, msemaji wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen, amesema muungano vamizi wa Saudia umetuma wapiganaji katika meneo ya vita ya Ma'rib.

Abdul Salam amesisitiza kuwa, jibu la ukiukaji wa usitishaji vita unaofanywa na Riyadh na Abu Dhabi litakuwa kali mno na kwamba vikosi vya jeshi na makundi ya kujitolewa ya wananchi wa Yemen viko tayari kukabiliana na uchokozi wowote.

Wakati huo huo Mehdi Al-Mashat, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesisitiza ulazima wa kufanikishwa usitishaji vita, kufunguliwa tena Uwanja wa Ndege wa Sanaa na bandari za Al-Hudaydah na kuondolewa mzingiro.

Usimamishaji vita nchini Yemen ulianza kutekelezwa tarehe pili mwezi huu wa Aprili kwa pendekezo la Umoja wa Mataifa lakini muda wote muungano vamizi hauheshimu usitishaji vita huo. 

4052124

Kishikizo: yemen ansarullah saudia
captcha