IQNA

Hali ya Waislamu India

Kinara wa wenye chuki dhidi ya Uislamu akamatwa India

21:04 - June 08, 2022
Habari ID: 3475350
TEHRAN (IQNA)- Kinara wa vijana wa chama tawala cha utaifa wa Kihindu cha Bharatiya Janata (BJP) nchini India amekamatwa kutokana na matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu Waislamu kwenye mitandao ya kijamii, polisi walisema Jumatano.

Harshit Srivastava, kiongozi wa vijana kutoka Chama cha Bharatiya Janata cha Waziri Mkuu Narendra Modi, alikamatwa katika mji wa Kanpur kufuatia mvutano wa kijamii wiki iliyopita wakati wa maandamano ya Waislamu kulaani maoni ya chuki dhidi ya Uislamu.
"Tulimkamata mwanasiasa wa eneo hilo kwa kutoa matamshi ya uchochezi dhidi ya Waislamu," Prashant Kumar, afisa mkuu wa polisi, na kuongeza kuwa watu wasiopungua 50 waliwekwa chini ya ulinzi kufuatia mvutano wa Kanpur.
Wakili wa Srivastava hakupatikana kwa maoni yake.
Machafuko ya hapa na pale yaliripotiwa katika maeneo mengine ya India baada ya matamshi yaliyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW ambayo yametolewa na msemaji wa BJP Nupur Sharma wakati wa mjadala wa televisheni.
Matamshi ya utovu wa adabu ya viongozi wawili wa chama tawala nchini India cha Bharatiya Janata (BJP) dhidi ya Bwana Mtume (SAW) yamekabiliwa na wimbi la malalamiko ya mataifa ya Kiislamu na Waislamu kwa ujumla ulimwenguni.
Ghadhabu za ndani zilizidi kushika kasi baada ya viongozi kutoka mataifa ya Kiislamu kama vile Qatar, Saudi Arabia, UAE, Oman, Indonesia, Malaysia, Pakistan, Iran na Afghanistan kuitaka serikali ya India kuomba radhi na kuwaita wanadiplomasia kupinga matamshi hayo dhidi ya Uislamu.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) yenye ushawishi mkubwa yenye wanachama 57 imesema katika taarifa yake kwamba matusi hayo yamekuja katika hali ambayo hali ya chuki dhidi ya Uislamu inazidi kuongezeka nchini India na unyanyasaji wa kimfumo dhidi ya Waislamu.
Wizara ya mambo ya nje ya India ilisema siku ya Jumatatu ujumbe na maoni ya kuudhi hayaakisi maoni ya serikali kwa njia yoyote.
Mzozo huo umekuwa changamoto ya kidiplomasia kwa Modi ambaye katika miaka ya hivi karibuni ameimarisha uhusiano mkubwa na mataifa ya Kiislamu yenye utajiri wa nishati.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya India imechukua hatua za kutaamaliwa na kutafakariwa kuhusiana na Waislamu na thamani za Kiislamu kama vile kubinya marasimu na shughuli za kidini za Waislamu, kupiga marufuku utoaji wa uraia kwa wahajiri Waislamu, kuondoa mamlaka ya kujitawala Kashmir na kunyamazia kimya vitendo vya ukatili na utumiaji mabavu vya wahindu wenye misimamo ya kufurutu ada dhidi ya Waislamu.

4062821

captcha