IQNA

Idi

Waislamu watasherehekea Idul Adha siku gani mwaka huu?

14:23 - June 27, 2022
Habari ID: 3475433
TEHRAN (IQNA)- Mwaka huu kulijitokeza hitilafu katika baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu kuhusu siku kuu ya Idul Fitr lakini inaelekea kuwa kutakuwa na hitilafu katika kuanisha siku kuu ya Idul Adha.

Inatazamiwa kuwa nchi za Kiislamuzitaafikiana kuhusu Siku Kuu ya Idul Adha ya mwaka huu wa 1443 Hijria Qamaria.

Kanali ya Al Jazeera imeripoti kuwa nchi za Kiarabu kama vile Saudia, Misri, Morocco na Jordan zimetaganza kuwa zitaanza kuitafuta hilali ya Dhul Hija tarehe 29 Juni kwa kutumia teleskopu maalumu wakati wa Magharibi. Kwa msingi huo inatarajiwa kuwa nchi hizo zitatangaza Alhamisi Juni 30 kuwa ni tarehe Mosi Dhul Hija.

Hatahivyo baadhi ya nchi kama vile Qatar na Kuwait zimetangaza kuwa zitaanza kuitafuta hilali ya Dhul Hija tarehe 28 Juni kwa sababu zilianza Dhul Qaada mapema kwa siku moja.  Kwa hivyo nchi hizo bila shaka zitangaza 29 Juni kuwa siku ya mwisho ya Dhul Qaada na kuanza Dhul Hija Juni 30.

Kwa hivyo yamkini baadhi ya nchi zikatangaza Idul Adha itasadifiana na Julai tisa na zingine Julai 10.

3479470

Kishikizo: idul adha siku kuu
captcha