IQNA

Qur’ani Tukufu inasemaje /16

Mwenyezi Mungu hana watoto na hii ndio sababu

23:34 - July 07, 2022
Habari ID: 3475472
TEHRAN (IQNA) - Kuna sababu mbili zilizotajwa katika Qur’an Tukufu ambazo zinathibitisha Mwenyezi Mungu hana watoto. Wafasiri wa Qur’ani Tukufu wanasema sababu hizi ziko katika aya ya 117 wa Surah al-Baqarah.

Uwezo wa Mwenyezi Mungu na jinsi Anavyotumia ni kati ya maswala ambayo watu wa dini wanatilia maanani na mtazamo wao kuhusu kadhia hii huunda imani na itikadi zao katika masuala mbali mbali. Uumbaji wa mbingu na ardhi umenasibishwa na sifa hii ya Mwenyezi Mungu. Katika aya  117 ya Surah al-Baqarah ya Qur’ani Tukufu tunasoma hivi:

بَدِيعُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰٓ أَمْرًۭا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ ١١٧

" Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapo taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa. "

Hii ni kwa njia ya jibu kwa wale walio katika Ukristo na Uyahudi ambao waliamini Mwenyezi Mungu ana watoto. Baadhi yao wangesema Uzair (AS) alikuwa Mwana wa Mungu. Wengine waliamini Nabii Isa au Yesu  kuwa alikuwa Mwana wa Mungu.

Allamah Tabatabai, katika tafsiri yake ya Qur’ani Tukufu ijulikanayo kama al-Mizan, ameichambua ayah ii na kusema imetoa sababu mbili katika kubainisha ni kwa nini Mwenyezi Mungu hana watoto. Ya kwanza ni kwamba kuwa Mwenyezi Mungu sio wa mwili na chochote kilicho mbinguni na dunia kinamtegemea. Kwa hivyo kunawezaje kuwa mtoto wake na kuwa na sifa zake?

Sababu ya pili, kwa msingi wa aya hii, ni kwamba Mungu ni Muumbaji wa Mbingu na Dunia. Anaunda kila kitu bila kuwa na mfano. Anachofanya sio msingi wa kuiga na sio hatua kwa kama vile wengine hufanya. Haitaji njia ya kufanya kile anachotaka kufanya. Mara tu atakaposema "kuwa", jambo hilo linatokea. Kwa hivyo hatuwezi kusema ana watoto kwa sababu kuwa na watoto kunahitaji taratibu maalumu za hatua kwa hatua.

Mapenzi  na irada ya Mwenyezi Mungu ni kwa msingi wa hekima na hivyo iwapo kitu kinaumbwa hilo huwa kwa mapenzi na irada ya Mwenyezi Mungu tu na hakuna hali nyingine inayohitajika.

Kulingana na tafsiri ya Nur ya Qur’ani Tukufu ya Sheikh Muhsin Qar’ati, aya hii inafikisha nukta mbili:

  1. Uumbaji wa Mungu daima ni wa asili (Badi'i)

2- Mungu anaweza kuunda uwepo wote katika sekunde moja tu ingawa hikma yake inahitajika kwamba kunapaswa kuwa na sababu za kupelekea kuwepo uumbaji wa taratibu au hatua kwa hatua.

captcha