IQNA

Utamaduni wa Kiislamu

Kila mwana kaligrafia Muislamu ana ndoto za kuandika aya za Qur'ani

19:35 - January 22, 2024
Habari ID: 3478235
IQNA - Mwandishi wa kaligrafia kutoka Misri ambaye amekamilisha uandishi wa Qur'ani Tukufu anasema kufikia mafanikio haya ni ndoto ya kila mwanakaligrafia Muislamu.

Ayman Nimir, mwana kaligrafia wa Misri na mwalimu anayeishii Alexandria, hivi karibuni alitimiza matarajio ambayo wengi katika taaluma yake wana ndogo ya kufikia nayo ni kuandika Qur'ani Tukufu.
Katika mahojiano na Masri Al-Yum, alieleza jinsi mafanikio haya yanawakilisha ndoto ya kudumu ya kila mwandishi wa kaligrafia.
Nimir alisimulia safari yake, akieleza kwamba alipoamua kuanza kazi ya kuandika kuandika aya zote za Qur'ani Tukufu kwa mtindo wa kaligrafia kwa mara ya kwanza, alitafiti kwa makini na kuandaa msingi kabla ya kuweka kalamu kwenye karatasi.
Licha ya juhudi za kujitolea, nakala ya kwanza, kwa sababu ya udogo wake, haikuweza kuchapishwa hata baada ya uchunguzi wa kina na Al-Azhar ili kuhakikisha usahihi wa Kiarabu na tahajia, ilisema ripoti hiyo.
Bila kukata tamaa, Nimir alichukua changamoto hiyo tena, wakati huu akichagua umbizo kubwa ambalo lingeweza kuchapishwa. Baada ya kukamilisha mchakato wa ufuatiliaji wa kina, alianza uchapishaji, safari iliyochukua miaka 11 ili kuchapisha Msahafu wenye maandishi yake.
Nakala hizi mbili za kipekee ziliandikwa kwa maandishi ya Naskh, na kwa mtindo wa Uthmaniya, na kuongeza kwenye historia tajiri ya Misri kama kitovu muhimu cha uandishi wa aya za Qur'ani Tukufu.

3486904

captcha