IQNA

Utamaduni

Kaligrafia ya Qur'ani Tukufu Msichana wa Kashmir yatambuliwa Kimataifa

22:20 - December 13, 2023
Habari ID: 3478030
IQNA - Msichana mdogo katika eneo la Kashmir linalotawaliwa na India amesifiwa kwa kazi yake ya kaligrafia ya Qur'ani Tukufu.

Sabreena Nabi mwenye umri wa miaka 20 anayetoka eneo la Charar-e-Sharief huko Budgam amepongezwa na wanakaligrafia dunaini kwa kuandika Surah Yusuf pamoja na tafsiri yake kwa Kiingereza na Kiurdu kwenye ukurasa wenye ukubwa wa mita 15.5.

Anatambulika kwa kazi nzuri kutoka katika Rekodi za Dunia za India na Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Ushawishi, ametajwa kuwa miongoni mwa wanakaligrafia bora zaidi duniani.

Sabreena alisema kwamba safari yake katika uandikaji wa maandishi ilianza kwa shauku ya kuandika kwa mkono na kujitolea kwake kulimpelekea kufanya kazi kubwa ya kunukuu sura nzima ya Kurani.

"Sikuzote nimependa kaligrafia na nimekuwa nikifanya mazoezi tangu nikiwa shuleni. Kwanza nilipata safu ndefu ya karatasi moja kutoka Delhi kwa sababu nilikuwa na shida kuipata hapa. Nilitumia karatasi yenye urefu wa mita 15.5 na kutafsiri Surah Yusuf katika Kiurdu na Kiingereza. Baada ya kuimaliza, juhudi zangu zilikubaliwa, na nikapokea tuzo kutoka kwa mashirika kadhaa,” aliambia shirika la habari la Kashmir News Observer (KNO).

Kulingana na Sabreena, ni mwanzo tu na anafanya kazi ya kuandika sura 30 za Qur'ani Tukufu kwa mkono.

captcha