Kwa mujibu wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS), warsha hiyo ni sehemu ya mradi unaoitwa "Maneno ya Nuru".
Inalenga kuhuisha na kuhifadhi kazi ya jadi ya uandishi wa Qur’ani Tukufu kwa mkono kama urithi wa kidini na kitamaduni.
Chuo kikuu hicho ambacho kinafungamana na idara hiyo kimewaalika wanafunzi, wasomi na wasimamizi kushiriki katika warsha hizo zitakazoanza baadaye mwezi huu.
Talal al-Kamali, rais wa chuo hicho, amesema warsha hizo zitafundisha, miongoni mwa mambo mengine, sheria na kanuni za uandishi wa Qur'ani.
Ameongeza kuwa nakala iliyoandikwa kwa mkono ya Qur’ani itazinduliwa siku ya Eid ya Mab’ath mwishoni mwa Januari 2025.
Ametoa wito kwa wanafunzi na wanataaluma kujiandikisha kwa ajili ya warsha na kuchangia mradi huo ambao ni wa kipekee katika historia ya chuo kikuu.
3490674