IQNA

Qur'ani Tukufu

Nakala ya Qur’ani iliyoandikwa kwa mtindo wa Uthman Taha kuchapishwa Iraq

21:23 - December 10, 2024
Habari ID: 3479886
IQNA - Nakala za Qur'ani iliyoandkwa kwa maandishi ya mtindo wa kaligrafia ya Uthman Taha itachapishw nchini Iraq kwa mara ya kwanza.

Kituo cha Dar-ul-Qur’ani chenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS), Karbala, Iraq imetangaza habari hiyo.

Misahafu hiyo inachapihwa zilichapishwa kwa amri ya Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, Mfawidhi wa haram hiyo , imesema taarifa hiyo.

Kituo cha Dar-ul-Quran na Jumba la Uchapishaji la Al-Warith zilishirikiana katika uchapishaji wa nakala hizo, kulingana na Sheikh Khayruddin al-Hadi, mkuu wa kituo hicho.

Alisema karatasi zenye ubora wa juu na wino wa kawaida zimetumika kuchapisha nakala 500.

Aliongeza kuwa kamati za sayansi na kiufundi zimesimamia hatua zote za uchapishaji.

Nakala hizo za Qur'ani hizo zitasambazwa bila malipo katika kongamano lijalo la Qur'ani kama sehemu ya juhudi za Astan za kuendeleza utamaduni wa Qur'ani, alisema.

Pia, Amal al-Matouri, ofisa mwingine katika kituo hicho, amesema kwamba wakati mradi kama huo unachukua angalau miezi sita kukamilika, kamati za kituo hicho zinaweza kuchapisha nakala hizo kwa siku 22.

Mtindo wa Uthman Taha ni mtindo wa kuandika Qur’ani Tukufu kwa maandishi ya Kufi kulingana na usomaji wa Warsh na usomaji mwingine ulioletwa na mwandishi wa kaligrafia wa Syria Uthman Taha.

4253139

Habari zinazohusiana
captcha