IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /28

Sura Al-Qasas: Nguvu ya Mwenyezi Mungu mkabala wa Utajiri na Nguvu za Mwanadamu

20:03 - August 29, 2022
Habari ID: 3475701
TEHRAN (IQNA) – Kumekuwa na makundi mbalimbali ya watu katika historia yote ambayo yameegemea juu ya uwezo na mali zao kusimama dhidi ya utawala wa Mwenyezi Mungu lakini wote wameshindwa kwani si wingi wa mali wala uwezo wa watu wenye nguvu unaoweza kukabiliana na nguvu za Mwenyezi Mungu.

Hii ni maudhui ambayo sehemu ya Surah Al-Qasas ya Quran Tukufu inazungumzia.

Ni sura ya 28 ya Qur’ani Tukifi.   Ni Sura ya Makki  ambayo ina aya 88 na imo katika Juzuu ya 20 ya Qur’ani Tukufu na ni Sura ya 49 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Jina Al-Qasas (hadithi) linatokana na hadithi za baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu zilizotajwa katika sura hii. Ni pamoja na kuzaliwa kwa Nabii Musa (AS), ndoa yake na binti wa Nabii Shuaib (AS), makabiliano yake na Firauni, na kisa cha Qaroon.

Pia inazungumzia visingizio ambavyo makafiri wa Makka walitoa kwa kukataa kuwa waumini.

Mfasiri maarufu wa Allameh Tabatabai, aliyeandika tafsiri ya Qur’ani Tukufu ijulikanayo kama Tafsir al Mizan, anasema lengo kuu la Sura hii ni kuahidi ushindi wa waumini waliokuwa kikundi kidogo na waliishi katika hali mbaya huko Makka kabla ya kuondoka mjini kuelekea Madina.

Sura hii iliyoteremka wakati Waislamu walipokuwa wakipatwa na matatizo, inasimulia kisa cha Musa (AS) tangu kuzaliwa kwake hadi ushindi wake dhidi ya Firauni na inawaahidi waumini kwamba wao pia watawashinda mafarao wa zama .

Inaahidi kwamba Taghut (katika istilahi ya Kiislamu inahusu wale wanaoabudu vingine badala ya Mwenyezi Mungu) wanaotegemea mali na uwezo wao kukabiliana na watu wa Mwenyezi Mungu watashindwa na waaminifu watairithi ardhi.

Hili linasisitizwa katika kisa cha Qaroon ambaye alikuwa na kiburi kwa sababu ya mali yake na elimu lakini akakabiliwa na mwisho kama ule wa Firauni.

Kwa mujibu wa Ufafanuzi wa tafsiri ya Qur’ani ijulikanayo kama Tafsir Nemouneh iliyoandikwa na Ayatullah Makarim Shirazi, hadithi za kushindwa kwa Firauni na Qaroon katika makabiliana na Musa (AS) zinaashiria ukweli kwamba matajiri au makafiri waliokuwa na nguvu huko Makka hawakuwa na uwezo wa kuzuia mpango wa Mwenyezi Mungu wa kuwaongoza waumini kwenye ushindi.

Baadhi ya aya nyingine za Surah Al-Qasas zinatoa mafunzo juu ya tauhidi, Siku ya Kiyama, umuhimu wa Qur’ani, uongofu na upotofu, na hali ya makafiri Siku ya Kiyama. Pia wanajibu visingizio vilivyotolewa na makafiri ambao walikataa kukubali mwaliko wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kwenye njia iliyonyooka.

Habari zinazohusiana
captcha