IQNA

Jinai za Israel

Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina inajiandaa kwa ‘Vita Vikubwa’ na Israel

19:22 - November 25, 2022
Habari ID: 3476147
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina imesema inajiandaa kwa "vita vikubwa" na utawala wa kikoloni wa Israel unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu, mwanachama wa harakati hiyo alisema.

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina Mohammed Al-Hindi ameyasema hayo kwenye Televisheni ya Al-Aqsa siku ya Jumanne  na kuongeza kuwa,"Suluhisho la kadhia ya Palestina ndio ufunguo wa suluhisho na utulivu kwa eneo zima,".

"Tunashikilia mapambano  hatujali mazungumzo ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala ghasibu wa Israel, ambao unadhani kuwa mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu yatamaliza harakati za mapambano. Hapana, makundi ya Palestina na wananchi wa Palestina wanajiandaa kwa vita hivyo vikubwa. "

Amesisitiza tena kwamba maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel huko al-Quds (Jerusalem) na Ukingo wa Magharibi u ndio "asili" ya mapambano na taifa la Palestina linalokaliwa kwa mabavu la Israel.

Mjumbe huyo mkuu wa Jihad ya Kiislamu alisisitiza kuwa Wapalestina wote katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, Palestina iliyokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 na Wapalestina walio  nje ya nchi, "wako pamoja na wapiganaji wa muqawama (mapamabano ya Kiislamu) katika mapambano yao dhidi ya uvamizi wa Israel.”

Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu uchaguzi wa hivi punde zaidi wa Israel, alisema: "Ulizidisha msuguano wa kijamii ndani ya jamii ya Israel. Kuna mgogoro wa kiuongozi. Netanyahu anajaribu kuunda serikali lakini wakati huo huo hataki kupoteza mikataba ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na baadhi ya madola ya Kiarabu."

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha