IQNA

Jinai za Israel

Hamas: Wapalestina hawataiacha Israel itekeleze njama zake dhidi ya Al Aqsa

16:38 - December 13, 2022
Habari ID: 3476241
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema Wapalestina katu hawatouruhusu utawala haramu wa Israel utekeleza njama na mipango yake michafu dhidi ya mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) na Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa ulio mjini humo.

Ismail Haniya amesema hayo katika hotuba aliyoitoa jana Jumatatu kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 35 tangu ilipoasisiwa harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.

Amesisitiza kuwa, wananchi wa Palestina wataendelea kusimama kidete dhidi ya njama za Wazayuni na kusisitiza kuwa, Quds itasalia kuwa kipaumbele cha kwanza kwa Hamas na taifa zima la Palestina katika zama na pahala popote.

Haniya amebainisha kuwa, kutumia muqawama na mapambano kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi na ukaliaji wa mabavu wa ardhi zao unaofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndiyo njia pekee ya kukabiliana na mipango ghalati ya Wazayuni.

Kiongozi huyo wa Hamas ameeleza bayana kuwa, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umo katika hali ya kudhoofika sana na katu hauwezi kuwa na ushawishi tena katika eneo la Asia Magharibi.

3481657

Habari zinazohusiana
captcha