IQNA

Jeshi la Yemen latekeleza operesheni kali dhidi ya meli iliyokuwa inaelekea 'Israel'

10:15 - July 10, 2025
Habari ID: 3480923
IQNA-Jeshi la Yemen limeshambulia meli nyingine iliyokuwa inaelekea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina 'Israel', ili kuwaunga mkono Wapalestina wanaokabiliwa na mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.

Katika taarifa yake jana Jumatano, Jeshi la Yemen limetangaza kuwa kikosi chake cha majini "kililenga meli ya 'ETERNITY C', iliyokuwa ikielekea bandari ya Umm al-Rashrash (Eilat) katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu", baada ya wafanyakazi wake kupuuza maonyo na wito uliotolewa na vikosi hivyo vya baharini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo ya kijeshi ilifanywa kwa "chombo kisicho na rubani na makombora sita ya baharini na ya balestiki."

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, meli hiyo "ilizama kikamilifu", na kwamba operesheni hiyo "imenakiliwa kwenye mikanda ya sauti na video. " Wafanyakazi hao, hata hivyo, "waliokolewa" na "kusafirishwa hadi mahali salama" na vikosi vya Yemen, imesisitiza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, marufuku iliyowekwa kwa meli zinazofungamana na Israel katika Bahari Nyekundu na Arabia bado ipo, ikionya makampuni dhidi ya kujihusisha na miamala au shughuli zinazohusisha bandari za Israel.

Jeshi la Yemen limesisitiza kuwa, kuunga mkono operesheni za Gaza na Palestina zitaendelea kwa kasi kubwa, na kwamba Wayemen watailinda nchi yao, na taifa lao kwa nguvu zote.

Tangu Israel ianzieshe mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza mwezi Oktoba 2023, majeshi ya Yemen yamefanya mashambulizi mengi kusaidia Wagaza waliokumbwa na vita, yakipiga malengo kote katika 'Israel', pamoja na kulenga meli zinazofungamana na Israel zinazopita katika Bahari Nyekundi.

Katika vita vinavyoendelea Gaza, utawala katili wa Israel umewauwa Wapalestina wasiopungua 57,680, wengi wao ni wanawake na watoto.

3493781

Kishikizo: yemen jeshi israel BAHARI
captcha