IQNA

Harakati za Qur'ani

Gaza Kaskazini: Wahifadhi 150 Wahudhuria Tukio la Kuhitimisha Qur'ani

11:06 - September 14, 2024
Habari ID: 3479432
IQNA - Zaidi ya wahifadhi wa Qur'ani wapatao 150 wanaume na wanawake kaskazini mwa Gaza walikusanyika kwa ajili ya kikao cha Qur'ani, ambao walisoma Qur'ani nzima nzima kwa kikao kimoja, pamoja na kuwepo vita vya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel dhidi ya eneo hilo.

Katika mpango huu, wahifadhi wa Qur'ani, waliogawanyika katika makundi ya wanaume na wanawake, walianza kusoma Qur'ani baada ya Sala ya Alfajiri hadi jioni kabla ya Sala ya Magharibi.

Awamu ya kwanza ya mpango huo ilifanyika miaka miwili iliyopita kwa usimamizi waNyumba ya Qur'ani na Sunnah ya Gaza, huku wahifadhi 581 wakike na wahifadhi Qur'ani wakishiriki.

Tukio hilo liliakisiwa pakubwa katika nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Kabla ya kuanza kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, wahifadhi 55,000 wanaume na wanawake wa kuhifadhi Qur'ani waliishi katika Ukanda wa Gaza. Wengi wa wahifadhi hawa wameuawa shahidi katika mashambulizi hayo.

Utawala wa Israel ulianzisha vita vyake vya kutisha dhidi ya Ukanda wa Gaza unaozingirwa tarehe 7 Oktoba mwaka jana kufuatia mashambulizi ya kulipiza kisasi ya vikosi vya kupigania ukombozi wa Palestina.

Uvamizi huo wa Israel umeua zaidi ya Wapalestina 41,000 na kujeruhi wengine zaidi ya 95,000, huku wengi wa wahasiriwa wakiwa ni wanawake na watoto.

4236364

Kishikizo: gaza qurani tukufu
captcha