IQNA

Qur'ani Tukufu

Qari wa Misri ambaye alisoma Qur'ani kwenye Redio ya Palestina kwa miaka mingi

17:46 - August 27, 2024
Habari ID: 3479337
IQNA – Mohamed Farid Alsendiony alikuwa qari mashuhuri wa Misri na ulimwengu wa Kiislamu, na mmoja wa kizazi cha kwanza cha maqari wenye kufuata mtindo wa Misri.

Ijumaa hii, Agosti 25, iliadhimisha kumbukumbu ya miaka 69 ya kifo chake, kulingana na tovuti ya El-Baladi.

Alsendiony alizaliwa mwaka 1912 katika kijiji cha Sendion katika Jimbo la Al-Qalyubia nchini Misri.

Alijifunza kusoma na kuhifadhi Qur'ani katika Maktab (shule ya jadi ya Qur'ani) kijijini kwao.

Baada ya kifo cha baba yake, aliondoka kwenda Cairo na punde akajulikana kama qari katika mji mkuu wa Misri.

Kisha akajiunga na Redio ya Misri kama msomaji wa Qur'ani.

Baada ya muda, alitumwa na Redio ya Misri kwenda Palestina kama qari mgeni. Alsendiony alisoma Qur'ani hapo kwa takriban miaka kumi.

Pia alisafiri katika baadhi ya nchi nyingine za Kiarabu kama Iraq, Jordan, Syria, na Kuwait kwa ajili ya kusoma Qur'ani.

Baada ya kukaliwa kwa mabavu Palestina mwaka 1947, alirejea Misri na kwenda katika Radio ya Cairo kufanya kazi huko kama qari. Walimtaka afanye mtihani ili kuthibitisha umahiri wake lakini alikataa na hakurudi tena redioni.

Kama msomaji mkubwa wa Kurani, anayejulikana katika ulimwengu wote wa Kiislamu, aliona kuwa haikubaliki kufanya mtihani ili kuthibitisha ujuzi wake.

Baada ya muda, alifungua nyumba ya kahawa ambapo alikuwa akisoma Qur'ani.

Alsendiony aliaga dunia mnamo Agosti 25, 1955. Ifuatayo ni faili ya sauti ya usomaji wake wa Aya ya 34 hadi 39 ya Surah Al-Qalam:

3489665

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu gaza
captcha