TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: "kuhudhuria kwa hamasa kubwa wananchi wa Iran katika maandamano ya Siku ya Quds Duniani bila shaka kumeyafanya maandamano ya mwaka huu kuwa moja ya maandamano yenye msisimko na taathira kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni na kuwapa faraja Mujahidina wanaopambana katika njia ya ukombozi wa Quds."

Takriban miaka 44 iliyopita tarehe 13 Ramadhani 1399 Hijria Qamaria sawa na tarehe 16 Mordad 1358 Hijria Shamsia, Imam Khomeini (MA), Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kwa mtazamo wa hekima na busara uliotambua ulazima wa kuwepo harakati ya wananchi duniani kwa ajili ya ukombozi wa Palestina na kutokomezwa dondandugu la saratani ya Israel aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds.