IQNA

Azimio la Siku ya Kimataifa ya Quds

Umoja ndio ufunguo wa kuangamiza njama za ubeberu wa kimataifa

16:22 - April 14, 2023
Habari ID: 3476865
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Iran walioshiriki katika maandamano ya leo ya Siku ya Kimataifa ya Quds wametangaza kuwa Umoja ndio ufunguo wa kushinda njama za ubeberu wa kimataifa.

Azimio la maandamano ya nchi nzima ya Intifadha na Siku Kimataifa ya Quds mwaka huu, limeeleza kuwa: Baada ya kupita miaka 44 tangu kutangazwa ubunifu wa kihistoria wa Imam Ruhullah Khomeini (RA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na uongozi wenye hekima wa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, sera na mikakati mibovu ya Marekani na washirika wake wa kikanda na kwengineko za kutaka kuudhaminia usalama utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina zimeshindwa na kugonga mwamba na sasa utawala huo wa Kizayuni unaelekea kusambatika na kutoweka kabisa kwa kasi kubwa kutokana na kukabiliana na harakati za kambi ya muqawama.

Washiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni "dhihirisho la umoja na azma ya Ulimwengu wa Kiislamu" katika kuunga mkono mapambano ya ukombozi ya Palestina na kukombolewa Quds Tukufu, wametangaza kuwa: Umoja na mshikamano wa Ulimwengu wa Kiislamu ndio ufunguo wa kushinda na kusambaratisha ubeberu wa kimataifa na njama za mabeberu.

Sehemu moja ya Azimio la Siku ya Quds imesisitiza udharura wa kimarishwa na kuungawa mkono muqawama na mapambano dhidi ya Uzayuni kama suluhu pekee la kadhia ya Palestina, ulazima wa kurejea wakimbizi wa Kipalestina katika nchi yao na kuitishwa kura ya maoni ya pande zote na huru ili kuainisha hatma na mustakabali wa Palestina.

Waandamanaji waliokuwa katika ibada ya Swaumu katika Siku ya Kimataifa ya Quds wamelaani hujuma ya kikatili iliyofanywa na jeshi la Israel dhidi ya Waislamu waliokuwa katika ibada ya Itikafu ndani ya Msikiti wa al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kusema kuwa mashambulio na kuvunjiwa heshima matukufu ya Waislamu vimefanyika ili kujinasua katika misukosuko ya Kisiasa na kiuchumi na machafuko ya ndani ya Israel na kutokana na hofu na kukata tamaa kwa utawala huo ghasibu kutokana na intifadha mpya na mapambano ya kizazi kipya cha Palestina.

Azimio la Siku ya Kimataifa ya Quds pia limelaani kimya na kutojali kwa jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu mbele ya jinai za kinyama za Wazayuni, na kuutaka Umoja wa Mataifa kusimamisha uanachama na kuufukuza utawala ghasibu, wa kibaguzi na unaoua watoto wa Israel katika umoja huo na  majukwaa mengine ya kimataifa.

4133895

Habari zinazohusiana
captcha