IQNA

Taarifa Muhimu

Maelfu ya wahadhiri wa Vyuo Vikuu Iran walaani ukatili wa Israel

22:19 - October 24, 2023
Habari ID: 3477783
TEHRAN (IQNA) –Wahadhiri 9,200 wa vyuo vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamelaani vikali ukatili wa utawala dhalimu wa Israel katika eneo la Palestina lililozingirwa la Ukanda wa Gaza.

Ofisi ya uwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika vyuo vikuu Iran imesamabza taarifa ya wahadhiri 9,200 ambao wamelaani vikali jinai za Israel huko Palestina.

Hii hapa ni matini kamili ya taarifa hiyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu wa Mashahidi na Wakweli

Operesheni ya fahari na adhimu ya "Kimbunga cha Al Aqsa", ambayo ilikuwa ni hatua huru na ya hiari ya makundi ya muqawama (wapigania ukombozi) na wananchi wa Palestina katika kutetea haki zao za asili na mashambulizi makubwa na ya kihistoria dhidi ya utawala wa Kizayuni, kwa mara nyingine tena ilithibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu katika Qur’ani Tukufu:

 أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ

Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui

Maneneo hayo yanaashiria imani ya uhakika, kuthibitisha kuhusu hofu ya uongo na nguvu bandia ya utawala huu wa Kizayuni unaoukalia kwa mabavu ardhi za Palestina. Oparesheni hii imeulazimisha utawala huo ghasibu kukabiliwa na kushindwa kusikoweza kurekebishwa. Bila shaka, oparesheni hii ni jibu halali kutoka kwa taifa linalodhulumiwa katika kutetea haki zake, na ni mapambano ya taifa dhidi ya wanyang'anyi na wavamizi wa ardhi ni haki isiyoweza kubatilishwa inayokubaliwa na watu wote watukufu na walio huru, wa dini yoyote na itikadi yoyote.

Katika upande mwingine, vitendo vya kikatili na vya kutisha vya utawala huo ghasibu wa Kizayuni daima vimewaweka watu madhulumu wa Palestina katika hali ya kukabiliwa na mauaji, jinai na ukatili, ambapo yote hayo hutegemea siasa za ubaguzi wa rangi ambazo ni msingi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika miongo kadhaa ya uhai wake. Rekodi mbovu ya utawala huu, tangu mwanzo hadi sasa, imejaa ukiukwaji mkubwa wa haki za kimsingi za Wapalestina, mauaji na kuvunjiwa heshima maeneo matakatifu, na inamkasirisha kila mtu huru. Kinachotokea leo huko Gaza na mashambulizi ya kikatili dhidi ya nyumba za makazi, miundombinu, misikiti, shule, vyuo vikuu, hospitali, na vikosi vya kutoa misaada na kukata mafuta, maji na umeme ni mifano ya wazi ya mauaji ya umati na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Je! Kwa nini watoto hawa wasio na hatia, wanawake wanaodhulumiwa, na wazee wasio na hatia wastahili kuburuzwa damu hadi chini kwa njia ya woga na ya kikatili namna hii? Wamefanya nini ili wawe wahasiriwa wa ulafi na uroho usioisha wa mbwa-mwitu hawa wanaowazia kwa uwongo kutawala ulimwengu na kuwa na udhibiti wa Mto Nile hadi Mto Frati? Je, wanaodai kutetea haki za binadamu wameshindwa kufahamu haki ya kuishi kwa watu hawa wasio na ulinzi, haki ya kutibu maumivu na majeraha yao ya kina, na haki ya kupumzika na kuishi chini ya paa la nyumba za mababu zao? Ufahamu huu umekuwa ni mgumu sana kwa wanaodai kutetea haki za binadamu kiasi kwamba hawawezi kutofautisha wavamizi wa Israel wenye kiu ya umwagaji damu kutoka kwa watu wasio na hatia wanaoshambuliwa. Chini ya bendera ya haki za binadamu wamenyamaza kimya katika tukio hili la kinyama au wanatoa wito kwa pande zote mbili kutulia na kujizuia na ghasia, au kumwaga machozi ya mamba kwa ajili ya ukandamizaji wa wavamizi wa Kizayuni na kuwaunga mkono. Hao wanaodai kutetea haki za binadamu wamekosa aibu kabisa na wanafuata mradi wa kuhamisha watu wa Palestina nje ya nchi yao, kujaribu kubadilisha muundo wa idadi ya watu katika ardhi hii.

Matukio ya hivi majuzi katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu yanaonesha kuwa sera ya kuwa na uhusiano wa kawaida na kuunga mkono utawala huo ghasibu si tu kwamba haitasaidia amani na usalama wa kieneo na kimataifa bali pia itauhimiza utawala huo kupuuza makumi ya maazimio ya Umoja wa Mataifa, na hivyo kuendelea na siasa zake za kibaguzi na uvamizi na kuendelea kutenda uhalifu wa kimataifa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu huku wakijifanya kuwa hawana hatia. Kwa bahati mbaya, utovu wa nidhamu na kutochukua hatua kwa nchi za Magharibi na Kiarabu na asasi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa dhidi ya ukiukaji huo mkubwa wa viwango na sheria za kimataifa na za kibinadamu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zimeufanya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa na jazba zaidi katika kuendeleza jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina. Inatarajiwa kwamba mashirika, mabaraza na taasisi zinazohusika na haki za kimataifa na za kibinadamu zitatekeleza majukumu yao ya kisheria na ya kibinadamu kwa kuacha sera ya kukaa kimya na kutochukua hatua na badala yake kutekeleza majukumu ya kutimiza haki za taifa la Palestina na kuwaadhibu wavamizi, na kujiepusha kushiriki katika jinai hizi zisizopingika ambazo ni fedheha kwa jamii ya wanadamu, na hivyo kwa jibu madhubuti na imara, sambamba na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni, kuuzuia utawala huu kuendelea na vitendo hivyo vya kutisha.

Sisi maprofesa wa vyuo vikuu vya Iran huku tukizienzi roho safi za mashahidi wa Kipalestina, tunawahurumia na tunatilia mkazo haki yao ya asili na ya kisheria ya kujilinda dhidi ya ukatili na jinai za kutisha za utawala ghasibu wa Israel. Kadhalika, tunatilia mkazo ulazima wa kuweko azma na hatua za dharura za kimataifa za kukomesha vitendo vya chuki dhidi ya binadamu vya utawala huu, na tunaamini kuwa utulivu na amani ya kudumu ya Palestina inaweza tu kuanzishwa baada ya kumalizika kukaliwa kwa mabavu, kurejea wakimbizi na uamuzi wa mfumo wa siku zijazo wa Palestina uchukuliwe kwa msingi wa kura ya maoni itakayowashirikisha Wapalestina wote, na hatimaye kuundwa kwa dola ya Palestina yenye mji mkuu wa Al-Quds al-Sharif.

Vile vile tunawaalika wasomi, wataalamu na wasomi wa ulimwengu hususan maprofesa wa ulimwengu wa Kiislamu kuchukua misimamo ya pamoja katika kulaani jinai hizo za kutisha, wawe ni sauti ya watu hao wanaodhulumiwa katika nyanja mbalimbali, na wasisahau wajibu wao kama wasomi katika kutetea haki za Wapalestina na kutoruhusu utawala huu kuwa janga la kikatili zaidi la binadamu kutokea mbele ya macho yao.

Kazi nyingine muhimu ni kufuatilia na kuhakikisha  utawala wa kigaidi na katili ya Kizayuni unakabiliwa na adhabu kali. Wanaadamu wote wenye fahamu na waadilifu wanakiri kwamba jinai iliyoenea ya mauaji ya watoto na wanawake wa Kipalestina katika siku chache hizi haipaswi kupita hivi hivi bila wahusika kuadhibiwa. Wahusika wote wa utawala huo ghasibu na wakiongozwa na kinara wao, mhalifu Netanyahu wanapaswa kufunguliwa mashitaka na kuadhibiwa na mahakama za kimataifa na zinazojitegemea.

Leo, wasomi wa vyuo vikuu wanaangaliwa kwa makini na walimwengi hatua yoyote ya kutosimama wasomi na wahadhiri wa vyuo vikuu, na wanaharakati wa kitamaduni na kijamii dhidi ya uvimbe huu wa saratani, yaani Israel, itarekodiwa katika historia. Ulimwengu unapaswa kujua kwamba watu wa Gaza hawako peke yao na Palestina daima imekuwa, ni, na itakuwa mwanachama wa ulimwengu wa Kiislamu.

و العاقبه لاهل التقوی و الیقین

Thousands of University Lecturers Slam Israeli Atrocities

Maprofesa kutoka vyuo vikuu kote ulimwenguni wanaweza kushiriki katika kampeni hii kwa kutuma maelezo yao kwa barua pepe, ikijumuisha jina lao na jina la chuo kikuu, kupitia barua pepe ifuatayo: info@iqna.ir

Habari zinazohusiana
captcha