IQNA

Jinai za Israel

Afisa wa Zamani: Lazima Jordan ijiandae kwa makabiliano ya kweli na Israel

22:41 - March 22, 2023
Habari ID: 3476743
TEHRAN (IQNA) - Jordan inapaswa kujiandaa kwa "makabiliano ya kweli" na utawala haramu wa Israel, afisa wa zamani wa Jordan amesema.

Naibu Waziri Mkuu wa zamani wa Jordan, Mamdouh Al-Abadi, alitoa maoni hayo Jumanne wakati akijibu matamshi ya waziri wa fedha wa mrengo wa kulia wa Israel Bezalel Smotrich ambaye alidai kuwa hakuna taifa kama Palestina alipokuwa amesimama kwenye jukwaa lililopambwa kwa ramani ya "Israeli Kubwa" iliyojumuisha Jordan.

"Israel inabidi iombe radhi rasmi kufustis matamshi ya [Smotrich]," Al-Abadi aliiambia Quds Press. Ametaja jibu la serikali ya Jordan kwa matamshi hayo kuwa dhaifu. "Tunapaswa kujiandaa kwa makabiliano ya kweli na Israel. Tunapaswa kuwa tayari kwa kuanza kuwasajili kwa lazima wanajeshi kwa sababu ajenda ya pande zote za Israel ni pamoja na kuikalia kwa mabavu Jordan."

Waziri huyo wa zamani hata alipendekeza kuwa uhusiano na utawala haramu wa Israel ukatwe kwa sababu matamshi ya Smotrich ni dhidi ya mapatano ya amani.

Kwa mujibu wa mkuu wa zamani wa Mahakama ya Kifalme ya Jordan, Jawad Anani, "Mustakabali wa uhusiano kati ya Jordan na Israel utaendelea kuwa mbaya maadamu Benjamin Netanyahu atakuwa waziri mkuu."

Kwa mara ya kwanza, aliongeza, wizara ya mambo ya nje ya Amman imeainisha matamshi kuhusu Jordan na Palestina ya waziri wa Israel kuwa yanakinzana na makubaliano hayo.

3482898

captcha