IQNA

Jinai za Israel

Bunge la Jordan lataka balozi wa Israel nchini humo atimuliwe

22:49 - March 22, 2023
Habari ID: 3476744
TEHRAN (IQNA)- Wawakilishi wa Bunge la Jordan wamepigia kura ya ndio pendekezo la kufukuzwa balozi wa utawala haramu wa Israel huko Amman wakilalamikia na kupinga hatua ya waziri wa fedha katika serikali ya mrengo wa kulia ya Israel, ambaye alizua utata mapema wiki hii.

Bezalel Smotrich Waziri wa Fedha wa Israel aliwashangaza wengi baada kuonyesha ramani ambayo ndani yake inaonyesha kuwa, sehemu ya ardhi ya na Palestina inayokaliwa kwa mabavu zimeunganishwa na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, kama ambavyo alikana uwepo wa watu wa Palestina.

Ahmad al-Safadi, Spika wa Bunge la Jordan amesema, Wabunge wa Bunge la nchi hiyo wanaitaka serikali ichukue hatua athirifu na yenye natija baada ya Waziri wa Fedha wa Israel kuonyesha ramani ambayo inaonyesha kuwa, sehemu ya ardhhi ya Jordan imeunganishwa na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Wakati huo huo, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jordan imelaani vikali hatua hiyo ya Bezalel Smotrich Waziri wa Fedha wa Israel na kuitaja kuwa ni ya kichochezi, isiyostahiki, inayokiuka ada za kimataifa na mkataba wa amani wa Tel Aviv na Amman.

Wakati Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jordan inamuita balozi wa Israel mjini amani na kulalamikia hatua ya Bezalel Smotrich, Wabunge wa Jordan wamepasisha kwa wingi wa kura pendekezo la kuutimuliwa balozi huyo kuutoka nchini Jordan.

Hatua ya waziri huyo imeendelea kulaaniwa vikali na wananchi wa Jordan katika maeneo mbalimbali hususan katika mitandao ya kijamii ambapo walio wengi wanasema, inaidhalilisha na kuivunjia heshima nchi yao.

4129464

captcha