IQNA

Dunia yaendelea kupinga mpango wa Israel wa kutwaa eneo la Ukingo wa Magharibi

14:14 - June 19, 2020
Habari ID: 3472878
TEHRAN (IQNA)- Nchi mbali mbali duniani zinaendelea kupinga utekelezaji wa mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupora eneo kubwa la Ukingo wa Magharibi.

Mkuu wa Sera za Nje za Umoja wa Ulaya ametahadharisha kwamba, utekelezaji wa mpango wa kutwaa eneo la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na Israel utakuwa na taathira mbaya katika uhusiano wa Ulaya na Isarel ambazo haziwezi kuepukika. Josep Borrell amekiambia kikao cha Bunge la Ulaya kwamba jumuiya hiyo inapinga mpango wa Israel wa kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuongeza kuwa, Brussels inaitaka Tel Aviv kujiepusha na hatua yoyote ya upande mmoja ya kutwaa sehemu ya ardhi ya Palestina. 

Borrel amesema kuwa, amewasilisha msimamo huo kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Waziri Ulinzi wa utawala huo, Benny Gantz. 

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, mpango huo unakiuka sheria za kimataifa na kuongeza kuwa, utakuwa na taathira mbaya kwa mchakato wa kutafuta suluhisho la mgogoro wa Palestina na Israel, amani ya Mashariki ya Kati na uhusiano wa Israel na Umoja wa Ulaya.

Maafisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamekubaliana kwamba, kuanzia tarehe Mosi Julai watayaunganisha maeneo ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi na ardhi zainazokaliwa kwa mabavu na utawala huo, suala ambalo limepingwa vikali na jamii ya kimataifa.  

3471733

 

captcha