Taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imesema: Ismail Haniyah, mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas, na mmoja wa walinzi wake wameuawa shahidi wakati makazi yao yalipopigwa mjini Tehran.
Sababu na undani wa tukio hili vinachunguzwa na matokeo yake yatatangazwa baadaye.
Wakati huo huo harakati ya Hamas pia imesema katika taarifa yake kwamba Ismail Haniyeh "ameuawa kutokana na hujuma ya kihaini ya Wazayuni dhidi ya makazi yake mjini Tehran."
Ismail Haniyeh alikuwa mjini Tehran jana (Jumanne) kushiriki katika sherehe za kuapishwa Rais wa Serikali ya Awamu ya 14 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
3489308