IQNA

Taarifa

Tamko la Iran kufuatia kuuawa shahidi Ismail Haniya

11:34 - July 31, 2024
Habari ID: 3479206
IQNA-Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametoa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) na kueleza kwamba, hapana shaka kuwa, damu ya mujahidi huyo haitapotea bure.

Nasser Kanani Chafi, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametoa mkono wa pole kwa taifa la Palestina, Harakati ya Hamas na makundi ya muqawama wa Palestina na mataifa na nchi zinazounga mkono kadhia ya Palestina.

Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kuwa mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) Ismail Haniyeh na mmoja wa walinzi wake wameuawa shahidi baada ya kushambuliwa makazi yao mjini Tehran.

Taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesema: Ismail Haniyeh, mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas, na mmoja wa walinzi wake wameuawa shahidi wakati makazi yao yalipopigwa mjini Tehran.

Hamas pia imesema katika taarifa yake kwamba Ismail Haniyah "ameuawa kutokana na hujuma ya kihaini ya Wazayuni dhidi ya makazi yake mjini Tehran."

Ismail Haniyah alikuwa mjini Tehran jana (Jumanne) kushiriki katika sherehe za kuapishwa Rais wa Serikali ya Awamu ya 14 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3489316

Habari zinazohusiana
Kishikizo: ismail haniya shahidi
captcha