IQNA

Muqawama

Yahya Sinwar achaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kisiasa wa Hamas

13:13 - August 07, 2024
Habari ID: 3479240
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imemteua Yahya Sinwar kuwa Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo ya muqawama, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Ismail Haniyah.

Shahidi Haniyah aliuawa kigaidi na utawala wa Kizayuni hapa mjini Tehran tarehe 31 Julai, siku moja baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian.

HAMAS imetangaza kuwa, imemteua Sinwar, ambaye amekuwa kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) katika Ukanda wa Gaza, kurithi mikoba ya Ismail Haniyah.

Ikumbukwe kuwa, mapema mwaka huu, Umoja wa Ulaya ulimuweka kiongozi huyo wa Harakati ya HAMAS katika orodha yake ya magaidi, kwa tuhuma za kufanikisha shambulizi la kushtukiza la Kimbunga cha al-Aqsa la Oktoba 7 mwaka uliopita. 

Hatua hiyo inamaanisha kuwa, nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimezuia eti mali za Sinwar katika nchi hizo. Aidha EU katika hatua hiyo, imewapiga marufuku wananchi wa nchi hizo za Ulaya eti kufanya muamala wowote na kiongozi huyo wa HAMAS.

Sinwar aliachiwa huru pamoja na Wapalestina wengine 1,000 mwaka 2011, katika mabadilishano baina ya mateka wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel, baada ya kuwa gerezani kwa miaka 22.

3489413

Habari zinazohusiana
captcha