Tovuti ya habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, mapema leo Alkhamisi asubuhi, Kiongozi Muadhamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameelekea kwenye viwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran na kuongoza Sala ya Maiti ya shahid Ismail Haniyeh, mwanajihadi shujaa wa kambi ya muqawama raia wa Palestina.
Baada ya Sala hiyo, kumefanyika shughuli ya maziko kutoka kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Tehran na kuelekea katika Medani ya Azadi yaani Medani ya Uhuru na Ukombozi, hapa Tehran. Kamanda huyo shujaa wa Palestina atazikwa mjini Doha, Qatar.
Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo nchini kote kufuatia kuuawa shahidi Kamanda Mwanajihadi, Ismail Haniya
Taarifa ya serikali ya Iran imesema kuwa, kuuawa shahidi Ismail Haniya, Kamanda Mwanajihadi na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kumeutia majonzi Umma wa Kiislamu, wafuasi wa njia ya fikra ya Muqawama na watetezi wa ukombozi kote duniani na kuongeza kuwa, mauaji ya kiongozi huyo yameongeza ukurasa mwingine wa faili chafu na la kuaibisha la jinai zinazofanywa na tapo la kihalifu na ghasibu la Kizayuni.
4229480