Khitma ya Ismail Haniya zitafanyika katika mfumo wa halqa ya Qur'ani mjini Tehran siku ya Ijumaa.
Khitma hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Swala (Mosalla) wa Imam Khomeini (RA) mjini Tehranbaada ya Swala za Maghribi na Ishaa, Mohammad Taqi Mirzajani, naibu mkuu wa Baraza Kuu la Qur'ani aliiambia IQNA.
Alibainisha kwamba Haniya alikuwa kiongozi mashuhuri wa mhimili wa muqawama na mtu ambaye alikuwa anaifahamu Qur'ani mbali na kuwa mhifadhi wa Kitabu hicho Kitukufu.
Mkuu huyo wa ofisi ya kisiasa ya Hamas alikuwa nafasi kubwa katika kukuza mafundisho ya Qur'ani miongoni mwa Wapalestina, jambo ambalo ni dhihirisho la upinzani mkali wa watu wa Ukanda wa Gaza dhidi ya ukatili wa utawala wa Kizayuni.
Mirzajani amebainisha kuwa Khitma hiyo ya Ijumaa itajumuisha usomaji wa Qur'ani unaofanywa na baadhi ya wataalamu wa Qur'ani wa Iran na hotuba za shakhsia kadhaa wa muqawama.
Haniyah aliuawa katika shambulizi dhidi ya makazi yake mapema Julai 31, katika mji mkuu wa Iran Tehran.
Alikuwa amefika Tehran kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei amesisitiza kuwa utawala wa Israel utakabiliwa na "adhabu kali" kwa kumuua kiongozi wa Hamas.
4230603