Hayo yako kwenye ripoti mpya ya shirika la kutoa misaada la Oxfam.
Ripoti hiyo imebaini kuwa utawala wa Israel umekuwa ukiwadhalilisha Wapalestina kwa kuwanyima maji na kuhatarisha maisha yao tangu Makubaliano ya Oslo ya 1993.
Halikadhalika Oxfam imesema takribani uharibifu kamili wa miundombinu ya maji na mifereji ya maji ya Gaza na jeshi la Israeli "umechangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa hali ya maisha huko Gaza".
Ripoti hiyo imeashiria hali mbaya iliyosababishwa na utawala katili wa Israel huko Gaza na kusema: "Usambazaji wa maji Gaza umepunguzwa kwa asilimia 94 ambayo ni chini ya lita 5 kwa siku kwa kila mtu, au chini ya bomba moja la choo, ambayo ni chini ya theluthi moja ya kiwango cha chini kinachopendekezwa katika dharura.
Wataalamu wengi wa kimataifa wa sheria na maji wanasema utawala katili wa Israel umeyatumia maji kama silaha katika mauaji ya kimbari kwa kuwanyima Wapalestina maji na usafi wa mazingira.
Kwa mujibu wa Oxfam, tangu kuanza kwa vita vya kikatili vya Israel dhidi ya Gaza mwezi Oktoba mwaka jana, maeneo matano ya miundombinu ya maji yameharibiwa kila baada ya siku tatu, wakati asilimia 70 ya pampu zote za maji taka na asilimia 100 ya mitambo yote ya kusafisha maji machafu pia imeharibiwa.
Kulingana na Oxfam, athari kwa afya ya umma huko Gaza imekuwa ya janga, huku visa vinavyoripotiwa vya magonjwa yanayosambazwa na maji vikiongezeka.
Tangazo la mapatano ya 'umoja wa kitaifa' wa Palestina linakuja zaidi ya miezi tisa baada ya Israel kuanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza kufuatia mashambulizi ya kushtukiza ya makundi ya wapiganaji wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.
Tangua Israel ianzishe mauaji ya kimbari ya Gaza, imewauwa takriban watu 39,006 wa Gaza, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na vijana. Wapalestina wengine 89,818 wamepata majeraha pia. China kwa muda mrefu imekuwa ikiunga mkono suala la Palestina.
3489248