IQNA

Jinai za Israel

Al-Azhar yatumai 2025 utakuwa mwaka wa ushindi, amani kwa watu wa Gaza

21:50 - January 01, 2025
Habari ID: 3479990
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha A-Azhar cha Misri kimebainisha matumaini kwamba mwaka wa 2025 utakuwa mwaka wa ushindi na amani kwa Wapalestina wanaokabiliwa na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.

"Ee Mwenyezi Mungu, mwaka mpya ujazwe na wema na huruma kwa watu wa Gaza na ushindi wao dhidi ya Wazayuni magaidi," Al-Azhar ilisema katika ujumbe wake kwenye Facebook.

Mwaka jana, watu wa Gaza waliteseka chini ya uvamizi wa kikatili wa adui magaidi walioua watoto wao wasio na hatia, ujumbe ulisomeka.

"Mwaka huu mpya uwe na makazi kwa watu hawa wasio na mavazi na wenye njaa ambao wako katika kivuli cha vita, na uwe mwaka wa neema tele baraka, amani na upatanisho kwa wakaazi wa Gaza, watu wa Palestina, na wengine kote ulimwenguni. ,” iliongeza.

Wakati huo huo, katika saa za kwanza za 2025, vyanzo vya ndani viliripoti mashambulizi mapya ya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina kote Gaza.

Ni pamoja na mashambulizi ya mizinga katika sehemu ya mashariki ya Khan Younis na sehemu ya magharibi ya Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Utawala wa Israel ulianza vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo la Palestina mwezi Oktoba 2023.

Vita vya mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na Wazayuni dhidi ya Gaza vimesababisha vifo vya Wapalestina 45,541 na kujeruhi 108,338 tangu Oktoba 7, 2023 ambapo aghalabu ya waliouawa ni wanawake na watoto

Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde, jeshi la Israel limewachinja watoto wachanga zaidi ya 1,000 katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha miezi 15 iliyopita. Takriban watoto 238 kati ya hao waliuawa mara tu baada ya kuzaliwa. Aidha, Israel imeua zaidi ya watoto 17,600 tangu Oktoba 2023 - mtoto mmoja kila dakika 30.

3491290

Habari zinazohusiana
captcha