Maafisa kadhaa akiwemo Mkuu wa Ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Vyuo Vikuu Hujjatul Islam Rostami, walihudhuria hafla hiyo.
Washindi wa kategoria tofauti walitambulishwa na kutunukiwa zawadi katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Tabriz cha Sayansi ya Tiba.
Jumla ya washindani 277 walishindania tuzo ya juu katika kategoria tofauti katika sehemu za wanaume na wanawake.
Walikuwa wametinga fainali baada ya kuonyesha utendaji bora katika raundi za awali.
Tarteel, usomaji wa Qur'ani, kuhifadhi Qur'ani katika viwango tofauti, usomaji wa du'a na usomaji wa mashairi ya kidini ni miongoni mwa kategoria za mashindano ya mwaka huu.
Jumla ya wataalamu 45 wa Qur'ani walihudumu katika majopo ya majaji katika sehemu za wanaume na wanawake.
Hafla hiyo ya kila mwaka huandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia na Wizara ya Afya na Sayansi ya Tiba.
Inalenga kukuza mafundisho ya Qur'ani miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
4236113