IQNA

Alievunjia heshima Qur’ani Urusi ashtakiwa kwa uhaini

21:56 - October 04, 2024
Habari ID: 3479535
IQNA – Mtu mmoja nchini Urusi (Russia) ambaye alikuwa amepewa kifungo cha jela kwa kuvunjia hesima Qur'ani Tukufu sasa anakabiliwa na shtaka jipya.

Nikita Zhuravel, ambaye alifungwa jela miaka 3.5 mwezi Februari kwa kuchoma  moto nakala ya Qur'ani nje ya msikiti katika mji wa Volgograd, kusini mwa Urusi, amefunguliwa mashtaka mapya kwa uhaini, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi ilitangaza Alhamisi.

Kulingana na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu, Zhuravel, 20, aliwasiliana na mjumbe wa Huduma ya Usalama ya Ukraine kupitia mtandaoni na "kutoa ushirikiano wake" kabla ya kuendelea kutuma video za ndege za kijeshi, treni zinazosafirisha zana za kijeshi, na harakati za magari ya kijeshi mnamo Machi 2023.

Chini ya sheria ya Urusi, adhabu ya juu kwa uhaini ni kifungo cha maisha.

Hapo awali Zhuravel alikamatwa Mei 2023 baada ya kuchapisha video yake akichoma moto nakala ya Qur’ani nje ya msikiti mmoja katika mji wa Volgograd kusini mwa Urusi. Wakati huo, wachunguzi walisema kwamba alikiri kufanya hivyo "kwa maagizo ya idara za ujasusi za Ukraine" kwa zawadi ya ruble 10,000 (€ 100).

Muda mfupi baada ya kukamatwa, Zhuravel alihamishwa hadi katika kituo cha mahabusu kabla ya kufunguliwa mashtaka katika jamhuri yenye Waislamu wengi ya Chechnya.

/3490132

Habari zinazohusiana
captcha