IQNA

Muqawama

Msaada usioyumba wa Yemen kwa Palestina

20:45 - December 29, 2024
Habari ID: 3479972
IQNA – Katika ulimwengu wa Kiarabu, ni Yemen pekee ambayo imesimama thabiti dhidi ya utawala wa Kizayuni na kwa mshikamano na Gaza na Palestina.

Msimamo huu, unaosukumwa na nia na hekima ya kiongozi wa Yemen na watu wake, umeunda fursa ya kuwawajibisha maadui wa jumuiya ya Kiislamu.

Hivyo, Yemen imekuwa chanzo cha hofu kwa wapinzani wake katika kumbukumbu za dunia na historia.

Ni mwaka mmoja na miezi mitatu tangu vita vya kikatili vilivyoanzishwa na utawala wa Israeli dhidi ya Gaza kuanza, na idadi ya watu katika eneo hili imepungua kwa zaidi ya nusu, kutokana na kuhama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Waisraeli. Hili ni janga jingine kwa Palestina.

Licha ya taswira za matukio ya kusikitisha kutoka Gaza kusambazwa kwa ulimwengu mzima, madola ya Magharibi yanaendelea kuunga mkono  utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuupa silaha za maangamizi ya umati, yakifumbia macho ukatili huu wote.

Hivi sasa utawala wa Kizayuni umepata kuhusu kuteka maeneo yote ya  Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuyaunganisha na maeneo mengine yote yaliyokaliwa kwa mabavu na hivyo  kupanua mzozo katika maeneo mengine, hasa Lebanon na Syria kwa nia ya kufikia ile ndoto potovu ya  "Israeli kubwa".

Yemen, ambayo yenyewe imejaa majeraha ya vita na kuzingirwa, tangu mwanzo wa uchokozi wa Kizayuni dhidi ya Gaza haijaacha msaada wake kwa Palestina. Kuongezeka kwa vita kumeweka muqawama wa Yemen katika makabiliano ya moja kwa moja na Marekani, na kusababisha ushindi kwa Yemen katika mzozo huu.

Kuangushwa kwa ndege ya kivita ya F-18 ya Marekani katika shambulio la angani la hivi karibuni nchini Yemen, kumepelekea kuibuke shaka kuhusu uwezo wa Marekani wa kudhibiti anga ya Marekani na uwezo wake wa kukabiliana na mashambulizi ya makombora na ndege za kivita zisizo na rubani kutoka Yemen.

Ndege za kivita za Jeshi la Wanamaji la Marekani pamoja na ndege za kivita za Uingereza mara kwa mara zimekuwa zikilenga maeneo tofauti ya Yemen. 

Katika kukabiliana uhasama huo, jeshi la Yemen, limetoa jibu thabiti kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani kushambulia meli za kivita za Marekani na washirika wake kama Uingereza na Ufaransa kwenye Bahari ya Nyekundu. 

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Yemen, idadi kubwa ya ndege za adui pia ziliondoka kwenye anga ya Yemen na kuelekea anga ya kimataifa katika Bahari Nyekundu ili kuilinda manoari ya USS Harry Truman baada ya kulengwa.

Jambo muhimu kuhusu kuangushwa kwa ndege ya kivita ya F-18 ya Marekani ni kwamba kutokana na mashambulizi makali na ya kiwango kikubwa ya Wayemen dhidi ya meli za kivita Marekani na Uingereza katika Bahari Nyekundu,  mifumo ya Marekani ya ulinzi wa angani na dhidi ya makombora ilikumbwa mkanganyiko. Marekani na waitifaki wake walikuwa wanatekeleza mashambulizi dhidi maghala ya silaha za Yemen, zikiwemo makombora na ndege za kivita zisizo na rubani ,ambazo zilikuwa zikishambulia manoari za kivita za Marekani na pia mashambulizi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Inadaiwa kuwa katika mashambulizi hayo, meli ya kivita ya Marekani ijulikanayo kama  USS Gettysburg ililenga kimakosa ndege aina F-18 ya Marekani na kuianisha madai ambayo kama tulivyosema yamekanusha na Jeshi la Yemen ambalo limesema ndilo lililotungua ndege hiyo.

Kwa vyovyote vile, tukio la kuangushwa ndege ya kisasa ya kivta ya F-18 linatilia shaka uwezo wa Marekani wa kuweza kukabiliana na mashambulizi yanayotekelezwa na majeshi ya Yemen.

Ni wazi kuwa Wayemen wanaweza kupanga mashambulizi yao dhidi ya meli za Marekani kwa njia ambayo itaibua matatizo na changamoto kubwa kwa Marekani na waitifaki wake hasa katika uga wa makombora na ndege zisizo na rubani.

3491251

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: yemen gaza
captcha