IQNA

Taaziya

Rais wa Iran: Kuuawa shahidi Sayyid Nasrallah kunaimarisha zaidi mti mwema wa Muqawama

20:34 - September 28, 2024
Habari ID: 3479503
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuuawa shahidi watu mashuhuri wa Kambi ya Muqawama, akiwemo kiongozi wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah, kunaimarisha zaidi mti mwema wa Muqawama na mapambano, na kuongeza kuwa: "Ulimwengu hautasahau kwamba amri ya shambulio hilo la kigaidi imetolewa New York."

Katika ujumbe wa pongezi na mkono wa rambirambi kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, watu wanaodhulumiwa na watu wote huru dunianI kutokana na mauaji ya kigaidi ya Sayyid Hassan Nasrallah, Rais Pezeshkiain amesema: Jamii ya kimataifa haitasahau kwamba amri ya kufanya shambulizi hilo kigaidi imetolewa huko New York, na Wamarekani hawawezi kujivua hatia ya kushirikiana na Wazayuni (katika uhalifu huo).

Katiika sehemu moja ya ujumbe wake, Rais Pezeshkian amesema: Tumejifunza kwamba uongozi ni wa Mwenyezi Mungu. Njia ya Mwenyezi Mungu haitabaki bila kamanda na kiongozi, na dunia hii itarithiwa na waja wema wa Mungu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba: Jamii ya kimataifa haitasahau kwamba amri ya shambulio hili la kigaidi imetolewa New York, na Wamarekani hawawezi kujinasua na dhima ya kushirikiana na Wazayuni.

Mwishoni mwa ujumbe wake, Rais Masoud Pezeshkian amesema: Hizbullah ya Lebanon itaendelea kung'aa kama jua kuliko wakati mwingine wowote, na hakuna shaka kwamba bendera ya mapambano dhidi ya dhalimu haitaanguka chini, na "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda, na ni Mwenye kulipiza kisasi".

 

4239203

Habari zinazohusiana
captcha